Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Philip Mpango leo Alhamisi, Februari 27, 2025 amewasili jijini Windhoek nchini Namibia ambapo anatarajia kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika maombolezo ya Kitaifa na Ibada ya kumuaga aliyekuwa Rais wa kwanza wa Namibia, Hayati Dk Sam Nujoma.