Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye, amefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka ya uasi, huku ombi la mawakili wake la kutaka ahamishiwe hospitalini kwa matibabu likikataliwa.
Besigye (68), wakati akiwa mahakamani leo Ijumaa Februari 21, 2025 ameonekana akiwa dhaifu na ameketi kwenye kiti mwendo baada ya mgomo wa kula alioufanya tangu Februari 12, mwaka huu akipinga kuzuiliwa kwake.