Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yametimia! Iraola atambulishwa Liverpool

Muktasari:

  • Liverpool ilimaliza Ligi Kuu ya NBC msimu uliomalizika wa 2025/2026 ikiwa katika nafasi ya tano kwenye msimamo.

Hayawi hayawi hatimaye yamekuwa. Baada ya tetesi za siku kadhaa, Liverpool leo Alhamisi, Juni 4, 2026 imemtambulisha rasmi Andoni Iraola kuwa meneja wake mpya.

Iraola amejiunga na Liverpool kwa mkataba wa miaka miwili akichukua nafasi ya Arne Slot aliyetimuliwa wiki iliyopita.

Mchakato wa kumnasa Iraola umeongozwa na Mkurugenzi wa Michezo wa Liverpool, Richard Hughes ambaye mwaka 2023 ndiye alimpeleka Iraola Bournemouth kabl ya kuhamia Liverpool mwaka 2024.

Liverpool inaamini kwamba Iraola ni chaguo sahihi kwao na wanadhani ni meneja ambaye atailetea mafanikio makubwa timu hiyo.

Iraola alikuwa na mwisho mzuri wa msimu uliopita baada ya kuiongoza Bournemouth kucheza mechi 18 mfululizo za Ligi Kuu England bila kupoteza.

Makali hayo yalipelekea Bournemouth imalize katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa EPL na kufanikiwa kupata fursa ya kucheza Europa League msimu ujao.

Iraola ameeleza kufurahishwa na yeye kujiunga Liverpool huku akiomba ushirikiano ili timu hiyo iweze kushinda mataji.

“Nimefurahi sana. Nimefurahi sana. Kwa sababu mara zote unajua Liverpool ni klabu kubwa na ni miongoni mwa timu kubwa zaidi duniani.

“Lakini nataka niseme kitu kwa mashabiki. Nataka niwe sehemu yenu. Nataka kupata haki ya kuwa sehemu yenu ili tufurahie pamoja,” amesema Iraola.