Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watanzania wanne kushuhudia bure Kombe la Dunia 2026

Muktasari:

  • Fainali za Kombe la Dunia 2026 zitafanyika Marekani, Canada na Mexico kuanzia Juni 11 hadi Julai 19 mwaka huu.

Wateja wanne wa benki ya CRDB wameshinda tiketi ya kushuhudia mbashara mechi ya fainali ya Kombe la Dunia nchini Marekani kupitia kampeni ya Fainali Ndo Mpango na TemboCard Visa”.

Washindi hao ni  Keneth Masana Bina, Arnold John Samugabo na Erick Harison Mlinga ambao wakazi wa Dar es Salaam na mshindi wa nne ni Gasper Melkiory Kavishe kutoka mkoa wa Morogoro.

Mbali ya washindi hao, pia wateja watatu wa benki hiyo wameibuka washindi wa Televisheni yenye ukubwa wa inchi 85, king’amuzi na kifurushi ambacho kitamwezesha mshindi kuangalia mechi zote za fainali hizo ambazo pia zitafanyika katika nchi ya Mexico na Canada kuanzia Juni 11 mpaka Julai 19.

Washindi hao ni Samson Mkumbo, Theresia Mawalla ambao ni wakazi wa Dar es Salaam na Eunice Masigati wa Dodoma.

Meneja mwandamizi wa kitengo cha Kadi cha benki ya CRDB, Karington Chahe  alisema kuwa wateja  hao wamepata ushindi huo baada ya kutumia kadi za TemboCard Visa Debit, Prepaid Card au Credit Card kufanya manunuzi  na kuingia moja kwa moja kwenye droo.

 “Nawapongeza  washindi wote na pia nawaomba wateja wa benki yetu kuendelea  kutumia TemboCard Visa Debit, Prepaid Card au Credit Card kufanya malipo katika huduma au bidhaa mbalimbali  ili kuingia moja kwa moja kwenye droo ili kuibuka washindi,” alisema Chahe.

Alisema kuwa kampeni hiyo inaendelea na kwa sasa wamebakiza washindi sita kwa ajili ya mechi za kombe la dunia na washindi saba wa televisheni ya inch 85 ambayo itakuwa pamoja na king’amuzi na kifurushi ambacho kitamwezesha mshindi kuona mechi zote za kombe la dunia.

“Lengo kubwa la kuendesha kampeni hii ni kuwazawadia wateja wetu na kuwaomba kuendelea kufanya manunuzi kupitia huduma zao,” alisema.

“Mpira wa miguu ni mchezo unaowaunganisha watu duniani kote bila kujali taifa, lugha au utamaduni wao. Kwa kulitambua hilo, sisi Benki ya CRDB tumeona ni muhimu kuwapa wateja wetu nafasi ya kuwa sehemu ya msisimko huo wa kimataifa kupitia mchezo huu pendwa duniani,” alisema.

Meneja mwandamizi wa kitengo cha Kadi cha benki ya CRDB, Karington Chahe (kulia) akizungumza wakati wa kutangaza washindi wanne wa kampeni ya Fainali Ndo Mpango na TemboCard Visa”. Wengine katika picha ni Esther Mhagama (katikati)ambaye ni mfanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja na Ali Selemani(DJ Ali B) ambaye ni balozi wa benki ya CRDB. 

Alisema kuwa kampeni hiyo itaendeshwa kwa kipindi cha miezi mitatu mpaka itakapohitimishwa tarehe 12 Juni 2026.

Alifafanua kuwa dunia kwa sasa inahamia kwenye mfumo wa malipo ya kidijitali hivyo Watanzania nao ni lazima waingie huko ili kuzitumia fursa zilizopo katika kununua au kuuza huduma na bidhaa kwani dunia imeshakuwa kama kijiji kwa watu kutoka popote duniani kununua huduma au bidhaa waitakayo bila kulazimika kuonana na muuzaji.

“Kampeni hii ni sehemu ya jitihada za Benki ya CRDB kuhamasisha matumizi ya malipo ya kidijitali, kuleta ubunifu katika huduma za fedha, na kuwazawadia wateja wetu kwa uaminifu wao.