Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waarabu wapewa dabi ya Simba, Yanga kesho

Muktasari:

  • Yanga wanaingia katika mchezo wa kesho wakiwa na kumbukumbuku ya kupoteza fainali ya Muungano huku Simba akiwa na kumbukumbu ya kufungwa na Yanga mara sita.

Dar es Salaam. Waamuzi kutoka Morocco ndio wamepewa jukumu la kusimamia dabi ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga SC itakayopigwa kesho saa 12 jioni Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.

Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi Kuu, Karim Boimanda amebainisha hay oleo Jumamosi Mei 2, 2026 huku akieleza kuwa uamuzi huo umezingatia kanuni za ligi.

Amesema uteuzi wa waamuzi wa nje haukutokana na maombi ya klabu yoyote, bali ni sehemu ya taratibu zinazoruhusiwa kikanuni.

“Waamuzi hawakuja kwa pendekezo la klabu kwa sababu kanuni inaruhusu. Kamati inapona kuna umuhimu inaweza kutumia waamuzi wa ndani au nje kulingana na uamuzi wake,” amesema Boimanda.

Walioteuliwa ni Hamza El Fareq mwamuzi wa kati akisaidiwa na Lahsen Agaou, Hamza Massiri na Mustapha Kechaf wote kutoka Morocco.

Boimanda pia amefafanua kuwa milango ya uwanja itafunguliwa kuanzia saa 7 mchana, huku akisisitiza kuwa mashabiki wenye tiketi pekee ndio wataruhusiwa kuingia, na vinywaji havitaruhusiwa uwanjani.

Kocha wa Simba, Steve Barker amesema timu yake inakabiliwa na mtihani mgumu kutokana na uimara wa Yanga katika safu ya ulinzi, akibainisha kuwa ushindi utategemea uwezo wa kutumia nafasi zitakazopatikana.

“Ili kushinda mechi ya kesho tunapaswa kufunga mabao, na sio rahisi kwa sababu Yanga wana safu nzuri ya ulinzi,” amesema Barker.

Ameongeza kuwa kikosi chake kipo katika hali nzuri na kina shauku ya kupata matokeo, huku akisisitiza kuwa ushindi utaipunguzia Simba tofauti ya pointi.

Beki wa Simba, Rushine De Reuck amesema wachezaji wamejipanga kuhakikisha wanawapa mashabiki wao furaha.

Naye, Kocha wa Yanga, Pedro Goncalves amesema kipigo cha fainali ya Kombe la Muungano dhidi ya Simba hakina uhusiano na mchezo wa ligi kuu, akisisitiza kuwa kila mashindano yana uzito wake.

Yanga ilipoteza 1-0 katika fainali hiyo iliyochezwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

“Ni mashindano tofauti, tunajiamini na tunaamini tunaweza kucheza vizuri kesho,” amesema Pedro.

Yanga itamkosa kiungo Mudathir Yahya ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu.

Pedro amesema kikosi kimezoea kucheza bila mchezaji huyo na kimejipanga vizuri kuelekea mchezo huo.

Beki wa Yanga, Mohamed Hussein amesema mchezo huo ni mkubwa na kila mchezaji amejipanga kuhakikisha anatimiza wajibu wake, akibainisha kuwa matokeo yataathiri mbio za ubingwa.