Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vurugu, ubaguzi vyatawala Sunderland ikiichapa Newcastle

Muktasari:

  • Licha ya vurugu hizo, Sunderland walifanikiwa kuibuka na ushindi baada ya Brian Brobbey kufunga bao la ushindi dakika ya 90.

Newcastle, England. Mchezo wa Ligi Kuu England kati ya Newcastle United na Sunderland ulisimamishwa kwa muda kwa mara ya kwanza kufuatia tukio la ubaguzi wa rangi, baada ya mchezaji wa Sunderland, Lutsharel Geertruida kuripoti kudhalilishwa na mashabiki wa Newcastle.

Tukio hilo limetokea mwanzoni mwa kipindi cha pili, ambapo mwamuzi Anthony Taylor alilazimika kusimamisha mchezo na kumuita nahodha wa Newcastle Kieran Trippier pamoja na viongozi wa benchi kujadili hali hiyo. Baadaye, Ligi Kuu England ilithibitisha kuwa hatua hiyo ilichukuliwa kufuatia malalamiko ya lugha ya kibaguzi iliyomlenga Geertruida.

Katika taarifa yake, ligi hiyo imesema tukio hilo litafanyiwa uchunguzi wa kina na kusisitiza kuwa ubaguzi wa rangi hauna nafasi katika soka wala jamii. Baada ya muda, mchezo uliendelea huku mwamuzi akizungumza pia na nahodha wa Sunderland Granit Xhaka kabla ya kuanza tena.

Mchezaji wa Sunderland, Lutsharel Geertruida ambaye anaripotiwa kufanyiwa vitendo vya kibaguzi katika mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Newcastle Machi 22, 2026. Picha na Mtandao

Licha ya vurugu hizo, Sunderland walifanikiwa kuibuka na ushindi baada ya Brian Brobbey kufunga bao la ushindi dakika ya 90, huku Chemsdine Talbi akisawazisha bao la awali la Anthony Gordon. Ushindi huo umeendeleza rekodi yao nzuri dhidi ya wapinzani wao, wakifikisha mechi 11 bila kupoteza.

Refa wa mchezo kati ya Sunderland na Newcastle, Anthony Taylor wakati akijaribu kutuliza hali baada ya mechi hiyo kusimama kufuatia tuhuma za ubaguzi dhidi ya mchezaji wa Sunderland, Lutsharel Geertruida. Picha na Mtandao

Hata hivyo, mchezo huo ulikumbwa na vurugu nje ya uwanja wa St James’ Park kabla ya kuanza, ambapo mashabiki wa timu zote walirushiana chupa na makopo. Ripoti zinaeleza kuwa mtu mmoja alipata huduma ya dharura ya kabla ya kukimbizwa hospitali, huku basi la Sunderland likiharibiwa kwa kurushiwa chupa.

Polisi nje ya Uwanja wa St Jame's Park, wakijaribu kuzuia vurugu zilizosababishwa na mashabiki wa Newcastle na Sunderland katika Ligi Kuu England. Picha na Mtandao

Polisi wa eneo hilo walithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kusema mtu mmoja alikamatwa kabla ya mchezo, huku wakiongeza ulinzi zaidi kuhakikisha hali ya usalama inadhibitiwa.