Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vigogo tisa Simba waifungia kazi Al Masry

Muktasari:

  • Timu inayotinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika inajihakikishia kitita cha Dola 750,000 kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Dar es Salaam. Simba ina kazi moja ngumu mbele yake Jumatano, Aprili 9, 2025 ambayo ni kuibuka na ushindi wa tofauti ya mabao matatu au zaidi dhidi ya Al Masry ya Misri  ili iweze kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kibarua hicho kigumu kwa Simba kimekuja kufuatia kupoteza mchezo wa kwanza uliofanyika huko Misri, Jumatano iliyopita kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Abderrahim Deghmoum na John Ebuka.

Kwa awamu tano zilizopita ambazo Simba ilifikia hatua ya robo fainali, ilishindwa kupenya na kuingia nusu fainali hivyo inaonekana haiko tayari kuendelea na nuksi hiyo msimu huu licha ya kupoteza mchezo wa kwanza ugenini.

Kudhihirisha hilo, vigogo tisa wa timu hiyo leo wameungana kwa pamoja kuwatangazia mashabiki wao kuwa wamefanya maandalizi ya uhakika na wana imani, Al Masry itapoteza kwa idadi kubwa ya mabao, matokeo ambayo yataivusha Simba na kuipeleka nusu fainali.

"Sisi tunapambana na tunaamini kwa uwezo wa Mungu tutashinda. Jambo moja sisi hatutishwi na mtu. wito wetu kwa Wanasimba kuiunga mkono timu yao kuelekea mchezo huo. Kwa kipekee tunamshukuru Mheshimiwa Rais wa Tanzania pamoja na viongozi wengine kwa ushirikiano wanaotupatia katika maandalizi," amesema mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu.

Mtendaji mkuu wa Simba, Zubeda Sakuru amesema,"Nafahamu wote kwa pamoja tuna hamu ya kupata matokeo katika mechi hii lakini matokeo haya kuyapata kwa kushinda na kufuzu. Sisi tumeweka mazingira mazuri ambayo yataiwezesha timu yetu kufuzu."

Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Simba, Issa Masoud amewahakikishia mashabiki wa timu hiyo kuwa uwezo wa kuitoa Al Masry wanao.

"Mpango wetu wa mwanzoni ilikuwa kumalizia hii mechi kule kwao lakini ikawa tofauti na sasa tumejipanga kumalizia hapa. Ujumbe wangu kwa Wanasimba wahakikishe hatufanyi vurugu lakini pia tushangilie muda wote wa mchezo.

Tukumbuke kwamba sisi tuna Tuzo ya Mashabiki Bora Afrika. Tumejulishwa pia CAF wataleta watu maalumu wa kusimamia mashabiki muda wote wa mchezo," amsema Masoud.

Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Swedy Nkwabi amesema kuwa mashabiki wa Simba wana nafasi kubwa ya kuisaidia timu kuitoa Al Masry.

"Kubwa niwaombe mashabiki na wapenzi wa Simba kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Mkapa. Tumekuwa tukivuka kwa mchango mkubwa wa mchezaji wa 12. Historia nyingi kwenye Uwanja wa Mkapa zinatuonyesha tulifanya vizuri.," amesema Nkwabi.

Nkwabi ameungwa mkono na mwenyekiti mwingine wa zamani wa zamani wa Simba, Hassan Dalali ambaye ametamba kuwa timu yao inaweza kufika hata fainali.

"Nataka kuwambia waarabu, tarehe 9 hawatoki. Hii ndio Simba, mtaona pale. Mimi naamini vijana, timu yetu ya Simba ina uwezo mkubwa sana na sisi tunataka kuchukua kikombe sio tu nusu. Fainali sisi tumeshaingia si tuliingia 1993, sasa hivi tunataka kikombe na kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu tutashinda," amesema Dalali.

Katibu mkuu wa zamani wa Simba, Hassan Hassanoo amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu hiyo huku akiwasihi kujiepusha na vurugu.

"Hatutakubali mtu yeyote kututoa nje ya mchezo. Zipo chokochoko zinaletwa na watu ambao kiuhalisia sio Simba lakini muda mwingine wanajifanya wanavaa jezi za Simba. Niwaombe mashabiki wetu siku hiyo kutokuwa wepesi wa kurejesha vurugu zozote. Simba tunaweza kuvuka na tunasema tuko tayari kuvuka kwenda hatua ya nusu fainali."- Katibu Mkuu wa zamani wa Simba," amesema Hassanoo.

Mfadhili wa zamani wa Simba, Azim Dewji amesema kuwa jukumu la kuitoa Al Masry ni la kila Mwanasimba.

"Hii mechi ni muhimu kwa kila mwanachama wa Simba. Nataka wanachama waelewe kuna tofauti gani ya Uwanja wa Mkapa na viwanja vingine. Uwanja wa Mkapa tunasema mtu hatoki, hatoki inamaanisha watu wote kujaza uwanja na mimi naona ushindi huu kwa asilimia 50 ni kujaza uwanja lakini pia kutengeneza historia kwamba wakati Simba inafuzu nusu fainali na wewe ulikuwepo uwanjani," amesema Dewji.

Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Simba, Dokta Seif Muba amesema, "Wachezaji tumewambia kwamba mashabiki wanataka ushindi lakini na wao wametutuma tuwambie mashabiki mjitokeze kwa wingi uwanjani na mshangilie mwanzo mwisho. Mnakumbuka kuna watu goli moja tu pale walishindwa lakini sisi tuna uwezo wa kumpiga mtu goli saba pale [Uwanja wa Mkapa]."