Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ujumbe wa Miloud kwa mastaa Yanga

Muktasari:

  • Yanga inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa imekusanya pointi 58 katika michezo 22.

Dar es Salaam. Kocha wa Yanga, Miloud Hamdi ametoa ahadi ya kufurahisha kwa wachezaji wake muda mfupi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Pamba Jiji, jana Ijumaa, Februari 28, 2025.

Hamdi amesema kuwa atahakikisha anatoa nafasi kwa kila mchezaji wa timu hiyo ili kuhakikisha analinda ubora wao na kuwaepusha na uchovu na majeraha.

Amesema kuwa kila mchezaji wa Yanga anastahili kupata nafasi ya kuitumikia timu hiyo na yeye kama kocha anatambua ubora wa kila mmoja hivyo atajitahidi kuwapa nafasi hadi pale msimu utakapomalizika.

“Siri yangu ni kuheshimu wachezaji wote na kama ninapoona mchezaji mmoja anastahili natakiwa kumpa muda wa kucheza na pia kama tukishinda, anatakiwa kuwa na dakika nyingi za kucheza.

“Natakiwa kuwatumia wachezaji wote. Kama tunataka kwenda hadi Mei, wachezaji wote wanatakiwa wawe tayari na ndio sababu nawapa nafasi kwa sababu wachezaji wanastahili. Hawapo hapa kwa ajili ya kufanya mazoezi tu bali wapo kuvaa jezi ya Yanga na kuwapa burudani mashabiki.

“Kama watakaa muda wote kwenye benchi wanawezaje kufanya hivyo? Hivyo kwa mimi hilo haliwezekani, natakiwa kutoa dakika nyingi kwa wachezaji wengi. Najitahidi kufanya hivyo,” alisema Hamdi.

Hamdi alisema anafurahia kuona wachezaji wake hawamuangushi kila anapowapa nafasi ya kucheza kwani wamekuwa wakionyesha kiwango bora ambacho kimekuwa kikichangia timu yake kupata matokeo mazuri.

Katika mchezo dhidi ya Pamba Jiji, mabao ya Yanga yalipatikana kupitia kwa Stephane Aziz Ki aliyefumania nyavu mara mbili na lingine moja lilifungwa na Chadrack Boka na kuifanya timu hiyo kufikisha pointi 58 zinazoifanya iendelee kuongoza msimamo wa Ligi Kuu msimu huu.

Kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga kilichoanza katika mchezo huo dhidi ya Pamba Jiji, kocha Hamdi alifanya mabadiliko matatu ya wachezaji kutoka katika kikosi kilichocheza dhidi ya Mashujaa FC na kuibuka na ushindi wa mabao 4-0.