Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TFF yakataa maombi ya Simba kuhusu Damaro

Kiungo mkabaji wa Yanga, Mohammed Damaro. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Simba wanapiga hesabu za kwenda Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) kupinga maamuzi hayo ya kamati ya sheria na hadhi za wachezaji.

Habari itakayowafanya mashabiki wa Yanga kucheka kwa furaha ni hii baada ya Shirikisho la Soka Tanzania kufanya maamuzi juu ya rufaa ya klabu ya Simba kuhusu kiungo wa mabingwa hao Mohammed Damaro.

Iko hivi, Simba iliwasilisha malalamiko mbele ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji juu ya uhalali wa Damaro ikipinga usajili wa kiungo huyo kwa madai unaifanya Yanga kuwa na wachezaji 13 wa kigeni badala ya 12 wanaotakiwa kikanuni.

Taarifa iliyotolewa na TFF imesema kamati hiyo imetupa shauri hilo la Simba ikieleza kuwa usajili wa Damaro hauna dosari kwa vile habanwi na kanuni zilizowasilishwa na klabu ya Simba.

Simba katika malalamiko yake ilidai usajili huo wa Camara ilikiuka kanuni ya 62(1) ya Ligi Kuu pamoja na kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Wakati wa kufanya maamuzi hayo, Simba iliwasilishwa na mwanasheria wa klabu hiyo Hosea Chamba aliyeambatana na mhasibu mkuu wa Stimu hiyo, Seleman Kaumbu.

Kufuatia maamuzi hayo bosi mmoja wa Yanga alisema hawakutaka kusumbuka kwenda kusikiliza shauri hilo kutokana na kukaa kwenye mlengo wa propaganda zaidi na sio uhalisia.

“Tulijua maamuzi yatakuwa hivyo kwa kuwa hiyo ndio haki na usahihi, unajua hawa wenzetu wanajua wanachokifanya, wanataka kututoa kwenye utulivu wa kimashindano, kiukweli hatukuwa na haja ya kuwapeleka watu wetu huko, tuliamini TFF itatoa haki kupitia kamati yake bila sisi kuwepo,”alisema bosi huyo.

Aidha baada ya Simba kupata maamuzi hayoinafahamika kwamba wekundu hao wanapiga hesabu za kwenda Mahakama ya Usuluhishi Michezoni (CAS) kupinga maamuzi hayo ya kamati ya sheria na hadhi za wachezaji.

“Hukumu imetoka muda huu, tunasubiri maamuzi ya wanasheria wetu, wakiona kama kuna haja ya kwenda mbele Simba itakwenda mpaka CAS kupata uamuzi wa mwisho,”alisema bosi huyo wa Simba ambaye ni mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi.