Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Taoussi aziwekea mtego Simba, Yanga

Muktasari:

  • Alisema ameikuta Azam ina mastaa wazuri wenye vipaji lakini bado zipo timu ambazo zinaweza kuwatikisa kiwepesi, hali ambayo hapendelei kuiona katika kikosi chake

Unaweza kuona kama ni mapema hivi, lakini sio kwa kocha wa Azam FC Rachid Taoussi ambaye rekodi za kikosi chake zinampa jeuri na kusema mpango wake mpya ni dhidi ya Simba na Yanga.

Azam kufikia sasa msimu imecheza mechi 12 za ligi, imeshinda nane, sare tatu na kupoteza moja dhidi ya Simba. Kati ya mechi ilizoshinda, iliizamisha Yanga 1-0 na kulipa kisasi cha kufungwa 4-1 na timu hiyo ya Jangwani katika mechi ya fainali ya Ngao ya Jamii.

Rachid ameanza kwa kufundisha kikosi hicho kwa mafanikio makubwa, tangu atue Azam amecheza mechi 11 akipokea kijiti kutoka kwa kocha Youssouph Dabo.

Akizungumza na Mwananchi, alisema kwake jambo la muhimu zaidi kwa sasa ni kutengeneza saikolojia ya wachezaji wake kujiona wana uwezo mkubwa.

Alisema ameikuta Azam ina mastaa wazuri wenye vipaji lakini bado zipo timu ambazo zinaweza kuwatikisa kiwepesi, hali ambayo hapendelei kuiona katika kikosi chake.

"Mpango nilionao ni mmoja tu wa kuhakikisha kikosi changu kinapita katikati ya Simba na Yanga, kwani hizo ndio timu pekee zinazoonekana tishio kwenye ligi lakini sio kwetu.

"Ni wazi kuwa Azam ni timu kubwa na ina wachezaji wenye viwango kama ilivyo kwa timu hizi mbili hivyo hatuna sababu ya kutufanya tusiwashinde."

Ikumbukwe kuwa Azam ndio iliyofungua mlango wa gundu kwa Yanga, baada ya kuwafunga bao 1-0 na baadaye timu hiyo ya wananchi kuchapwa 3-1 na Tabora United na kisha kulala 2-0 nyumbani dhidi ya AL Hilal katika Ligi ya Mabingwa Afrika. 

Msimu uliopita Azam chini ya kocha Dabo, katika mechi 12 za kwanza ilishinda mechi 10, sare moja na kupoteza mmoja, hivyo kwa rekodi hizo kikosi cha kocha Dabo hakina tofauti kubwa na anachofanya Rachid kwa sasa katika mechi za kwanza.