Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Stori ya kusisimua ya Ronaldo, Szoboszlai wakipambana leo

Muktasari:

  • Szoboszlai leo anaingia uwanjani kukiongoza kikosi cha Hungary kama nahodha kwenda kuchuana na Ureno ya Ronaldo, ambaye pia ni nahodha.

BUDAPEST, HUNGARY. Kudumu muda mrefu kwenye soka la kiwango cha juu kumemfanya Cristiano Ronaldo kuandikisha rekodi za kipekee kabisa katika mchezo huo wenye mashabiki wengi duniani.

Ronaldo, 40, bado anapambana ndani ya uwanja kwa kucheza soka la kiwango cha juu, lakini sasa atakutana na mchezaji ambaye aliwahi kuwa maskoti katika moja ya mechi alizocheza huko nyuma. Miaka 16 iliyopita, wakati huo Dominik Szoboszlai, akiwa na umri wa miaka minane alikuwa maskoti kwenye mechi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2010 iliyokutanisha Hungary na Ureno, ambapo Ronaldo alikuwa akicheza tayari.

Szoboszlai aliingia kwenye Uwanja wa Ferenc Puskas na alisimama hatua chache tu kutoka alipokuwa amesimama shujaa wake, supastaa Ronaldo.

Szoboszlai huyu ndiye yule wa kikosi cha Liverpool. Na usiku wa leo, Jumanne, anaingia uwanjani kukiongoza kikosi cha Hungary kama nahodha kwenda kuchuana na Ureno ya Ronaldo, ambaye pia ni nahodha wa miamba hiyo ya Ulaya. Mechi hiyo ni ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 kwa upande wa Uefa, ikiwa ni raundi ya kwanza kwenye Kundi F.

Ronaldo kipindi ambacho Szoboszlai alikuwa maskoti, alikuwa na umri wa miaka 24 na alikuwa ametoka kuweka rekodi ya dunia kwenye uhamisho aliponaswa na Real Madrid kwa ada ya Pauni 80 milioni mwaka 2009.

Na sasa Ronaldo akiwa veterani akicheza soka lake huko Saudi Arabia, mkali Szoboszlai anaonyesha ubora wake huko kwenye Ligi Kuu England akichezea kikosi cha mabingwa, Liverpool.

Akizungumzia fursa hiyo ya kucheza dhidi ya shujaa wake, Szoboszlai alisema: "Nilicheza dhidi ya wachezaji wengi sana mahiri, lakini sijawahi kucheza dhidi yake (Ronaldo).

"Tangu utoto wangu amekuwa shujaa wangu na sasa umefika wakati wa kucheza dhidi yake. Natumaini hii itakuwa safi."

Kitendo cha Ronaldo kudumu kwenye soka kwa muda mrefu kimemfanya kukabiliana na wachezaji wasiotarajiwa kabisa. Straika huyo wa Al-Nassr, aliwahi kucheza pamoja na kocha wa sasa wa Manchester United, Ruben Amorim kwenye mechi nane za timu ya taifa ya Ureno.

Na alicheza pia na mtoto wa mchezaji ambaye amembadili kwenye kikosi cha Ureno wakati alipoanza kuibukia kuitumikia timu hiyo. Ronaldo sasa anacheza pamoja na Francisco Conceicao kwenye kikosi cha Ureno kwenye mechi tisa tofauti, huku mchezaji huyo ni mtoto wa Sergio Conceicao aliyewahi kucheza na Ronaldo 2003.

Sergio Conceicao, 50, alicheza mechi 56 za kimataifa kwenye kikosi cha Ureno na alistaafu 2003 baada ya Ronaldo kuibukia kuichezea timu hiyo. Kipindi hicho Ronaldo alikuwa na umri wa miaka 18 na mechi yake ya kwanza Ureno alicheza miezi miwili kabla ya Conceicao Sr kustaafu.