Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Stars hairudii makosa kwa Sudan

Muktasari:

  • Mchezo huo hautakuwa na kiingilio chochote kwani Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema mashabiki wataingia bure uwanjani, kuiunga mkono Stars ili iweze kulipa kisasi dhidi ya Sudan na kutinga raundi inayofuata dhidi ya Waethiopia.

Taifa Stars ina uhakika wa kucheza fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) 2025, sambamba na Kenya na Uganda, lakini hiyo haiwafanyi wabweteke wakati leo jioni watakapovaana na Sudan katika mechi ya marudiano ya raundi ya kwanza ya mechi za kuwania fainali hizo.

Stars ilipoteza bao 1-0 ugenini wikiendi iliyopita huko Mauritania, lakini leo watakuwa na nafasi ya kulipa kisasi wakati zitakaporudiana kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam na mshindi wa jumla atasonga mbele raundi ya pili kuvaana na Ethiopia iliyopewa ushindi wa chee kutokana na Eritrea kujitoa.

Mchezo huo hautakuwa na kiingilio chochote kwani Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema mashabiki wataingia bure uwanjani, kuiunga mkono Stars ili iweze kulipa kisasi dhidi ya Sudan na kutinga raundi inayofuata dhidi ya Waethiopia.

Tangu irejee nchini kutoka Mauritania, Stars ilikuwa ikijifua kwenye viwanja wa TRA, Kurasini na baaadaye KMC uliopo Mwenge kujiweka fiti kwa mchezo huo na mapema kocha mkuu wa timu hiyo, Bakar Shime pamoja na wachezaji walisema wamejianda vya kutosha kuhakikisha wanapata matokeo mazuri nyumbani.

"Ni mchezo mgumu na hasa baada ya kupoteza ugenini, Wasudan watakuja wakitaka kulinda ushindi wao nasi tukitaka kulipa kisasi ili tusonge mbele kwa hatua inayofuata, bahati tumeshagundua makosa na tumejipanga kufanya vizuri na tupo nyumbani," alisema Shime.

Tanzania, Kenya na Uganda ndio wenyeji wa fainali hizo za CHAN za mwakani zikazofanyika kabla ya fainali za Afcon 2025 zitakazopigwa Morocco, kisha nchi hizo tatu za Afrika Mashariki kuja kuandaa Afcon 2027.

Katika mechi ya leo Stars itaendelea kuwategemea wachezaji wengi wa timu ya Vijana U20 iliyobeba ubingwa wa Cecafa na kukata tiketi ya Afrika U20 mbalimbali wa wazoefu wa Ligi Kuu Bara kama kina Valetino Mashaka, kipa Aishi Manula, Ame Ibrahim, Edgar William, Seleman Mwalimu na wengineo.