Simba yatua kwanza Kwa Mkapa,Yanga yafuata

Muktasari:
- Yanga inahitaji ushindi au sare dhidi ya Simba katika mechi yao leo, Jumatano, Juni 25 ili itwae ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu wakati Simba inahitaji ushindi tu iweze kuchukua taji.
Mambo yanazidi kuchangamka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam ambako dakika chache baadaye, Yanga itakabiliana na Simba katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Timu zote mbili zimeshawasili uwanjani hapo tayari kwa mchezo huo.
Simba imewasili Uwanja wa Mkapa,ikiwa timu ya kwanza kufika ikipishana na Yanga kwa dakika mbili kisha ikapokelewa na shangwe na mashabiki wa timu zote mbili.
Simba imefika uwanjani hapo saa 9:26 Mchana,ikiwa kwenye basi lao kubwa, huku mbele kukiwa na pikipiki ya askari wa Jeshi la Polisi.
Wakati Simba ikifika uwanjani hapo, mashabiki wachache wa timu hiyo,walilipuka kwa shangwe wakipata uhakika wa timu yao kucheza mechi hiyo.
Sio Simba pekee hata mashabiki wa Yanga nao waliishangilia kuwaona watani wao wakiwasili uwanjani hapo.
Hata hivyo Simba ilipoingia tu, Yanga wakafuata nyuma kwa dakika mbili baadae ambapo waliingia saa 9:28 alasiri wakiwa kwenye mabasi mawili madogo aina ya Coastel yenye rangi nyeupe.
Nyuma ya basi hilo ilipofika saa 9:35 alasiri, Yanga ikaingiza basi lao maalum la wachezaji likiwa halina mtu yeyote likisindikizwa na pikipiki ya king'ora