Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yatoa msimamo ishu ya Kibu

Muktasari:

  • Klabu ya Simba imesema itamchukulia hatua za kinidhamu Kibu Denis kwa kushindwa kuwasili kambini kwa maandalizi ya msimu mpya, licha ya kuongezewa mkataba hadi 2026 na kulipwa stahiki zake zote.

Tabora. Uongozi wa Klabu ya soka ya Simba umesema umepanga kumchukulia hatua za kinidhamu kiungo wake mshambuliaji, Kibu Denis kutokana na kushindwa kuwasili kwenye kambi ya timu hiyo kwaajili ya maandizi ya msimu ujao.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo leo Julai 23, 2024 imeeleza kuwa mchezaji huyo amekuwa akitoa Sababu ambazo hazifiki mwisho.

"Klabu ya Simba inautaarifu umma kuwa mchezaji wetu Kibu Denis Prosper hajaripoti kambini kwaajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mwaka 2024-2025," imeeleza na kuongeza,

"Tunapenda kuutarifu umma kuwa Simba tulimuongezea mkataba Kibu, mkataba wa miaka miwili zaidi utakaoisha Juni 2026 na kumlipa stahiki zake zote za kimmkataba,"

"Hata hivyo mchezaji huyu amekuwa akitoa sababu kadhaa wa kadha zinazomfanya kushindwa kuripoti kambini, kutokana na utovu huu wa nidhamu klabu itamchukulia hatua stahiki za kinidhamu na umma utapewa taarifa."

Kikosi cha Wanamsimbazi kipo nchini Misri kilikoweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Pia, Simba jana ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya El-Qanah ikipata ushindi wa mabao 3-0, yakifungwa na nyota wapya Jean Ahoua anayetajwa kuwa mrithi wa Clatous Chama na kiungo mkabaji Augustine Okejepha.


Endelea kufuatilia Mwananchi.