Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yapanda kileleni, Ateba akitupia mbili

Muktasari:

  • Kichapo hiki kimeifanya Tabora kubaki nafasi ya tano ikiwa na pointi 25, baada ya kucheza michezo 16 ya ligi hiyo.

Beki wa Simba Shomary Kapombe amefunga bao la tatu kwanye ligi msimu huu baada ya kuiongoza timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tabora United, huku timu hiyo ikirejea kileleni mwa msimamo.

Huu ulikuwa mchezo wa kwanza wa Simba wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara baada ya kumaliza wa kwanza ikiwa kileleni mwa msimamo.

Katika mchezo huu uliopigwa Uwanja wa Al Hassan Mwinyi Tabora, Simba imekuwa timu ya kwanza kati ya nne kubwa za juu kuifunga Tabora kwenye michezo yote miwili ya msimu huu, baada ya kupata ushindi kama huo mechi ya mzunguko wa kwanza, lakini timu hiyo ikiwa imeibuka na ushindi dhidi ya Yanga, Azam na kutoka sare na Singida BS.

Katika mchezo huo, ambao Simba ilionekana kucheza kwa kasi ilifanikiwa kujipatia bao la kwanza kupitia kwa Lionel Ateba katika dakika ya 14, ambapo alirejea na kufunga la pili katika dakika ya 35 kwa mkwaju wa penalti likiwa ni bao lake la saba kwenye ligi msimu huu, moja nyuma ya kinara wa mabao kwenye ligi, Elvis Rupia ambaye amefunga mabao manane hadi sasa.

Kipindi cha pili, Tabora ilionekana kuonyesha kiwango bora kuliko kile cha kwanza, lakini kosa moja walilofanya mabeki wake liliwagharimu ambapo katika dakika ya 66, Kapombe aliifungia timu yake bao la tatu, likiwa ni la tatu kwake kwenye ligi msimu huu.

Pamoja na bao hilo, bado yupo nafasi ya pili kwa mabeki waliofunga mabao mengi akiwa nyuma ya Ibrahim Hamad Bacca wa Yanga aliyefunga mabao manne hadi sasa.

Simba imerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kufikisha pointi 43 ikiwa na pointi moja mbele ya Yanga ambayo juzi iliichapa Kagera Sugar mabao 4-0.

Sasa Simba imefunga mabao 36, ikiwa nyuma ya Yanga kwa bao moja ibaada ya mabingwa hao watetezi kufunga mabao 37, lakini ikiwa imeruhusu mabao matano na Yanga sita.

Kichapo hiki kimeifanya Tabora kubaki nafasi ya tano ikiwa na pointi 25, baada ya kucheza michezo 16 ya ligi hiyo.

"Tunaipongeza Simba kwa kuwa imepata ushindi, lakini kwetu bado tuna kazi ya kufanya kwenye michezo yetu inayokuja," Anicet Kiazayid kocha Tabora United.