Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yaendeleza ubabe Ligi kuu

Simba imeendelea kufanya vizuri baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ken Gold kwenye uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam.

Mabao ya Simba yamefungwa na Leonel Ateba ambaye amefunga mawili dakika ya 34 akifunga kwa mkwaju wa penati baada ya Awesu Awesu kuchezewa vibaya ndani ya eneo la hatari.

Zilipita dakika 10 Leonel Ateba akafunga bao lingine kwa mpira wa kichwa ambao ulimpita golikipa wa Ken Gold, Castor Muhagama na kuingia wavuni, Simba ikiandika bao la pili na kuondoka ikiwa inaongoza kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili kilianza Simba ikifanya mabadiliko kadhaa ambapo alitoka kiungo, Fabrice Ngoma akimpisha Augustine Okejepha, Mzamiru Yasin alimpisha Yusuph Kagoma, Joshua Mutale akiingia kuchukua nafasi ya Awesu Awesu huku Kelvin Kijili akimpisha Mohamed Hussein.

 Leonel Ateba anafikisha mabao matano ndani ya Simba sawa na Jean Ahouwa ambao wapo nyuma kwa mabao mawili dhidi ya Elvis Rupia anayeongoza akiwa na mabao saba kwenye Ligi kuu.

Baada ya ushindi dhidi ya Ken Gold, Simba inasogea mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi kuu ikiwa na pointi 31 nyuma ya vinara Azam FC ambayo inaongoza Ligi ikiwa na pointi 33 wakati Ken Gold inabaki nafasi ya 16 ikibuluza mkia ikiwa na pointi sita.

Mchezo unaofuata Simba itakuwa ugenini kwenye uwanja wa Kaitaba dhidi ya Kagera Sugar Desemba 21, 2024 wakati Ken Gold itacheza kwenye uwanja wa CCM Liti dhidi ya Singida Black Stars Desemba 24, 2024.