Simba Queens yaivuruga Kisarawe mabao 8-0

Muktasari:
- Mashindano hayo yamezinduliwa rasmi leo na yatachezwa katika vituo mbalimbali nchini.
Ligi Ndogo ya Wanawake imeanza leo asubuhi katika Uwanja Karume, Dar es Salaam ambapo madada wa Simba Queen wamewachapa Kisarawe Queens mabao 8-0.
Mjini Dodoma Alliance Academy ya Mwanza imeifumua Mapinduzi ya Njombe 1-0. Pia jioni hii mechi nyingine zinaendee kwa mujibu wa Katibu wa Chama cha Soka Wanawake Tanzania (TWFA), Someo Ng’itu.
Endelea kufuatilia ukurasa huu ili kupata matokeo mbalimbali ya mechi kwenye viwanja mbalimbali kuhusu soka la wanawake kwa mechi zinazoendelea.