Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Scholes amkataa Carirck Manchester United, Ancelotti atajwa

Muktasari:

  • Scholes anaamini Carrick bado hajathibitisha kama anaweza kuiletea United mataji makubwa.

Manchester, England. Nguli wa zamani wa Manchester United, Paul Scholes, amesema kocha anayefaa zaidi kuinoa klabu hiyo ni Carlo Ancelotti, huku akihofia uzoefu wa Michael Carrick katika kushindania mataji makubwa.

Manchester United inatarajiwa kumteua kocha wa kudumu majira ya kiangazi baada ya Carrick kuchukua mikoba kwa muda kufuatia kuondoka kwa Ruben Amorim mapema mwaka huu.

Carrick ameanza vyema, akishinda mechi sita kati ya saba za kwanza za Ligi Kuu England na kutoka sare moja, rekodi inayomuweka sambamba na makocha bora kuwahi kuanza kwa kasi katika historia ya ligi hiyo.

Ushindi dhidi ya Crystal Palace mwishoni mwa wiki uliifanya United kupanda hadi nafasi ya tatu na kujiimarisha katika mbio za kumaliza ndani ya tano bora.

Hata hivyo, licha ya mwanzo huo mzuri, Scholes anaamini Carrick bado hajathibitisha kama anaweza kuiletea United mataji makubwa.

Nyota wa zamani wa Man United, Paul Scholes (kushoto) mwingine ni kocha wa zamani wa Real Madrid na sasa timu ya taifa ya Brazil, Carlo Ancelotti ambaye anapigiwa upatu kuja kuinoa Klabu hiyo ya Old Trafford baada ya Kombe la Dunia. Picha na Mtandao


Ampigia chapuo Ancelotti

Akizungumza Scholes amesema Ancelotti ambaye kwa sasa ni kocha wa timu ya taifa ya Brazil ndiye chaguo bora.

Amesema Ancelotti ana uzoefu wa kushinda mataji na uwezo wa kuwafanya wachezaji wajiamini, jambo ambalo United inalihitaji kwa sasa.

“Huyo ndiye mkamilifu kwa Manchester United. Ana uzoefu wa kushinda na ana haiba ya kiuongozi,” amesema Scholes.

Hata hivyo, ameibua swali kama umri wa Ancelotti unaweza kuwa changamoto, akisisitiza kuwa United inahitaji kocha mwenye uzoefu na uwepo mkubwa wa kiuongozi.

Meneja wa Manchester United, Michael Carrick,.ambaye anaiongoza Klabu hiyo kwa muda baada ya kuondoka kwa Ruben Amorim. Picha na Mtandao


Uzoefu wa Carrick watiwa shaka

Carrick amewahi kuifundisha Middlesbrough kati ya mwaka 2022 na 2025 kabla ya kurejea Old Trafford. Lakini Scholes anaona tofauti kati ya kufundisha Championship na kuinoa klabu yenye presha kubwa kama United.

“Je, tunaweza kumuona Michael akishinda Ligi Kuu England? Bado sijui,” amesema.

Ameongeza kuwa uongozi wa klabu hiyo unapaswa kuamua kama wanahitaji fundi wa mbinu au kocha anayejali zaidi mahusiano ya wachezaji.

Scholes alimrejea pia kocha wa zamani wa United, Ole Gunnar Solskjaer, akisema alikuwa mzuri katika usimamizi wa wachezaji lakini alihoji kama alikuwa na uzoefu wa kutosha kushinda mataji makubwa.

Kwa sasa, mustakabali wa benchi la ufundi la Manchester United unaendelea kuwa gumzo, huku macho ya mashabiki yakielekezwa kwa uongozi wa klabu hiyo kuona kama watampa Carrick nafasi ya kudumu au watajaribu kumshawishi Ancelotti kurejea katika soka la klabu baada ya Kombe la Dunia.