Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sare zaivusha Cape Verde 32 bora 

VERDE Pict

Muktasari:

  • Timu zote zimemaliza dakika 90 zikitengeneza nafasi moja bora lakini zikashindwa kuzitumia lakini Cape Verde kwa mara ya kwanza ikacheza mechi ambayo iliongoza kwa kumiliki mchezo.

Cape Verde imefanikiwa kutinga hatua ya 32 bora katika Fainali za Kombe la Dunia 2026 kwa aina yake baada ya kumaliza mechi tatu za makundi bila ushindi ikiambulia sare zote.

Cape Verde imemaliza mechi yake ya tatu kundi H dhidi ya Saudi Arabia kwa sare isiyo na mabao lakini ikatosha kuipeleka hatua inayofuata.

Timu zote zimemaliza dakika 90 zikitengeneza nafasi moja bora lakini zikashindwa kuzitumia lakini Cape Verde kwa mara ya kwanza ikacheza mechi ambayo iliongoza kwa kumiliki mchezo.

VERD -1

Kipa wa Cape Verde, Josimar José Évora Dias maarufu Vozinha, kwa mara nyingine akaibeba tena timu hiyo, akifanya kazi nzuri ya kuokoa mashambulizi matatu, huku mama yake mzazi akiwa jukwaani akimshuhudia.

VERD -2

Cape Verde ambayo ilianza mashindano hayo kwa kuilazimisha suluhu Hispania, ikatoka sare mchezo wa pili dhidi ya Uruguay timu hizo zikifungana mabao 2-2 kabla ya kumaliza na Saudi Arabia matokeo yakiwa 0-0.

Matokeo hayo yameipeleka Cape Verde kwenye hatua ya 32 bora ikimaliza nafasi ya pili ikiwa na pointi tatu kwenye kundi H likiongozwa na Hispania yenye pointi saba, wakati Uruguay ikiwa ya tatu na pointi mbili sawa na Saudi Arabia iliyomaliza nafasi ya nne ambazo zimeondoshwa mashindanoni.