Sababu Pacome kuachwa Dar, apewa siku tano

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua.
Muktasari:
- Pacome Zouzoua wa Yanga hakuondoka na timu kwenda Afrika Kusini kutokana na pasipoti iliyokuwa imejaa.
Dar es Salaam. Baada ya sintofahamu ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua kutoongozana na kikosi cha timu hiyo kwenda Afrika Kusini, Mwananchi linafichuliwa sababu iliyomfanya asiwe sehemu ya kikosi hicho ni ishu ya pasipoti.
Pacome amepewa siku tano kumaliza tatizo hilo kabla ya kuungana na wenzake Afrika Kusini ambapo mchakato umeanza leo Julai 2024 kuishughulikia.
Awali kiungo huyo alikuwa pamoja na kikosi hicho tangu mazoezi hayo ya Pre Season kuanza, lakini juzi wakati timu uinaoondoka hakuwepo na ilishindikana kufahamika kwa mapema, hadi ilipoelezwa tatizo lililoomzuia asiondoke na wenzake.
"Sababu ya Pacome kutoondoka pamoja na wenzake ni pasipoti yake ilikuwa imejaa, hivyo inatakiwa arejee nchini kwao Ivopry Coast kwa ajili ya kupata nyingine," kilisema chanzo hicho kutoka Yanga na kuongeza;
"Kutokana na umuhimu wa sababu yake, uongozi umempa siku tano, ili akamilishe kila kitu, kisha ajiunge na wenzake Afrika Kusini, ambako watakaa wiki mbili na kurejea nchini kujiandaa na mambo mengine."
Ndani ya hizo wiki mbili watakazokuwa Sauzi, Yanga itashiriki mashindano mawili ambayo ni Mpumalanga Cup na Toyota Cup, ikitarajiwa kuvaaba na timu za FC Augsburg ya Ujerumani na TS Galaxy kisha kumalizana na Kaizer Chiefs inayonolewa na kocha wa zamani wa Wanajangwani, Nasreddine Nabi.