Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rashford kubaki Barcelona bado pagumu

RASHFORD Pict

Muktasari:

  • Mchezaji huyo wa kimataifa wa England alijiunga na klabu hiyo ya Hispania dirisha lililopita la majira ya kiangazi  kwa mkopo wa msimu mmoja.

Barcelona, Hispania. Barcelona imeshafanya uamuzi wao juu ya hatma ya mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford anayecheza kwa mkopo katika kikosi chao.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa England alijiunga na klabu hiyo ya Hispania dirisha lililopita la majira ya kiangazi  kwa mkopo wa msimu mmoja.

Tangu atue Rashford ameonyesha kiwango bora, akifunga mabao matatu na kutoa pasi tano za mabao  katika mechi 10 alizocheza hadi sasa.

RASH 01

Kwa mujibu wa ripoti kutoka Hispania, klabu hiyo yenye maskani yake huko Catalonia iko tayari kutumia kipengele kilichopo katika mkataba wake kinachowapa nafasi ya kumnunua mazima ikiwa watahitaji.

Hata hivyo, dau la Pauni 26 milioni linalohitajika ili kufanikisha hilo linaonekana kuwa kubwa kwa Barca kutokana na hali yao ya kiuchumi.

Barca ipo katika hali ngumu kifedha ambayo inawazuia kusajili wachezaji kwa uhuru, kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.

Hali hiyo imesababishwa na sheria ngumu za La Liga  kuhusu usawa wa kifedha ambazo zinaeleza timu haitakiwi kutumia zaidi ya kile inachoingiza.

Ili kukamilisha dili hilo kwanza,  Rashford huenda akalazimika kukubali kupunguzwa mshahara wake wa Pauni 325,000 kwa wiki, pia taarifa kutoka tovuti ya  Tribal Football, inaeleza kwamba Barca inaweza kujaribu kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Manchester United, kuona kama inaweza kupunguziwa bei.

RASH 02

Ikiwa hatua hizo zote zitafeli, Barca inaweza kuomba tena kumpata Rashford kwa mkopo wakati ikijiweka sawa kimahesabu ili kumnunua baadae.

Staa huyu ana mkataba na Man United hadi mwaka 2028, jambo linaloifanya timu hiyo kutaka kiasi chochote inachohitaji kwa sababu mkataba bado ni mrefu.