Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rashford akubali kujiunga na Aston Villa

Muktasari:

  • Rashford amefanikiwa kufunga mabao 138 akiwa na  United baada ya kucheza michezo 426 na sasa anaangana na timu hiyo.

Staa wa Manchester United Marcus Rashford, anatarajiwa muda wowote kuanzia sasa kufanya vipimo vya afya ili kujiunga na Aston Villa kwa mkataba wa mkopo.

Staa huyo amekuwa hana uhusiano mzuri na kocha mpya wa Manchester United, Ruben Amorim, kuanzia kocha huyo ametua kwenye timu hiyo na sasa anajiandaa kujiunga na Villa.

Mkataba wa mchezaji huyo na Villa utakuwa wa mkopo hadi mwishoni mwa msimu na kama timu hiyo itaridhishwa na dili hilo basi itamsajili moja kwa moja kwa kitita cha pauni 40 milioni.

Taairifa kutoka Daily Mail, inasema kuwa Rashford na Villa wameshakubaliana kila kitu na kilichobaki ni staa huyo kusaini mkataba tu.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa mshambuliaji huyo ambaye ameitumikia timu ya Taifa ya England mechi 60 anatarajiwa kuendelea kupokea kitita chake kilekile cha mshahara cha pauni 350,000 kwa wiki na mkataba wake na United unatarajiwa kumalizika Juni 2028

Taarifa inasema kuwa Villa watalipa asilimia 70 ya mshahara huo, huku mambo mengine yakiwa makubaliano yao na Man United.

Rashford hajafanikiwa kuitumikia United kuanzia Desemba baada ya kuanza kuvurugana na kocha Ruben Amorim.

Hadi anatarajiwa kujiunga na Villa staa huyo mwenye miaka 27 amekosa michezo 12 baada ya kocha wake kulalamika kuwa staa huyo hajitumi uwanjani.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Rashford kuitumikia timu nyingine tofauti na United baada ya kukaa kwenye timu hiyo kuanzia akiwa na miaka nane.

Rashford amefanikiwa kufunga mabao 138 akiwa na  United baada ya kucheza michezo 426 na sasa anaangana na timu hiyo.