Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PSG yaiondoa Madrid, kuivaa Chelsea fainali

Muktasari:

  • Chelsea, waliotinga fainali kwa kuifunga Fluminense ya Brazil katika nusu fainali nyingine, sasa watalazimika kuwa makini kila idara.

New Jersey, Marekani. Klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) imethibitisha ubora wake katika soka baada ya kuichapa Real Madrid mabao 4-0 kwenye nusu fainali ya Klabu Bingwa Dunia iliyochezwa katika uwanja wa MetLife, New Jersey.

Wakiwa na mastaa wao wote wakiongozwa na Ousmane Dembélé, Fabian Ruiz na Gonçalo Ramos, vijana wa kocha Luis Enrique waliitawala mechi hiyo tangu dakika ya kwanza, huku wakitumia makosa ya mabeki wa Real Madrid kuandika mabao mawili ndani ya dakika tisa.

Dembélé alifunga bao moja na kusaidia moja, huku Ruiz akifunga mawili na Ramos akihitimisha karamu ya mabao dakika ya 88. Kwa matokeo hayo, PSG sasa itavaana na Chelsea katika fainali itakayopigwa Jumapili, Julai 13.

Hii ilikuwa mechi ya mwisho kwa kiungo mkongwe wa Real Madrid, Luka Modric, aliyeingia dakika chache na kushuhudia timu yake ikizidiwa kila idara. Kocha wa Real, Xabi Alonso, amekiri kikosi chake kilizidiwa ujanja.

"Hii PSG imejengeka kwa muda, sisi bado tunajifunza. Tumefika nusu fainali, lakini tuna kazi kubwa ya kujenga timu inayoelewana," amesema Alonso.

Kwa upande wake, Enrique amesema: "Tupo katika kipindi maalum. Tunataka kutengeneza historia kwa kushinda taji hili. Tunaiheshimu Chelsea lakini tupo tayari."

Real Madrid walicheza chini ya kiwango licha ya kuwa na mastaa kama Jude Bellingham, Antonio Rudiger, Vinicius Junior, Kylian Mbappe na Thibaut Courtois, ambaye hata hivyo aliokoa michomo kadhaa hatari.

Chelsea, waliotinga fainali kwa kuifunga Fluminense ya Brazil katika nusu fainali nyingine, sasa watalazimika kuwa makini kila idara kama wanataka kuizuia PSG inayotisha kwa kasi na ufundi mkubwa.