Nyota wa soka Brazil atupwa jela miaka minne na nusu kwa ubakaji

Muktasari:
- Nyota huyo aliyekipiga katika klabu maarufu kama Barcelona na PSG amehukumiwa hii leo katika mahakama moja huko nchini Hispania.
Barcelona, Hispania. Nyota wa zamani wa Brazil, Dani Alves amehukumiwa kwenda jela miaka miaka minne na nusu kwa ubakaji.
Nyota huyo aliyekipiga katika klabu maarufu kama Barcelona na PSG amehukumiwa hii leo Alhamisi Februari 22, 2024 katika mahakama moja huko nchini Hispania.
Shirika la Habari la AFP limesema Alves ametupwa jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka msichana mdogo katika klabu ya usiku huko Barcelona Desemba 2022.
Pia, jarida la Forbes limeeleza kwamba Alves alimbaka msichana huyo bafuni katika eneo la VIP ya klabu hiyo iitwayo Sutton.
Alves awali alikana kumjua mwathiriwa huyo wakati alipohojiwa kwenye televisheni. Hata hiyvo baadaye, alikiri kufanya naye ngono lakini alidai kuwa walikuwa wamekubaliana.
Alves aliliambia gazeti la La Vanguardia kwamba awali aliamua kudanganya kwa sababu alihofia mkewe Joanna Sanz angeamua kuachana naye.
