Nyomi la mashabiki lawapokea mastaa Yanga

Baada ya mastaa wa Yanga kutoka katika Uwanja wa Ndege, wamepokelewa na nyomi la mashabiki ambao wamejaa barabarani wakiisindikiza timu yao.
Bila kujali jua kali mashabiki wa Yanga wameonyesha hawana shoo ndogo baada ya kujitokeza kuwapokea mastaa wao waliokuwa wametoka kwenye mechi ya fainali ya Kombe la CRDB.

Kikosi hicho ambacho kitazunguka maeneo makuu manne ambayo ni Tazara,Karume,Msimbazi na kumalizika Jangwani kinasherehekea msimu baada ya kutwaa makombe matano.
Mashabiki hao wengi wameamua kutembea kwa miguu huku wengine wakikimbia barabarani huku wakiimba kwa furaha.

Mashabiki hao wamekuwa wakikimbia mbele, nyuma na pembeni ya basi maalumu lililowabeba mastaa wa kikosi hicho pamoja na viongozi wao.
Ikumbukwe Yanga msimu huu imebeba makombe matano ambayo ni Toyota, Kombe la Muungano, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na CRDB.