Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyakati mbaya zaidi kwa Yanga

Dar es Salaam. Hakuna utata kwamba kila mmoja kwa sasa anasifia soka la kikosi cha Yanga kinachonolewa na kocha Miguel Gamondi, baada ya kucheza mechi sita za mashindano.
Katika mechi hizo sita za mashindano, Yanga imeonekana kufunga zaidi mabao kwenye kipindi cha pili kuliko cha kwanza.
Yanga imefunga mabao 19 katika mechi sita za mashindano yake yote hadi sasa, huku kipindi cha kwanza ikifunga mabao manne pekee na 15 yakiwa kwenye kipindi cha pili.
Yanga imecheza mechi mbili za Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC ikishinda 2-0 na suluhu dhidi ya Simba kisha (Yanga) ikafungwa kwa mikwaju ya penalti 3-1.
Mabao ya mchezo dhidi ya Azam FC yalifungwa kipindi cha pili, dakika ya 84 na Stephen Aziz Ki na la pili likifungwa na Clement Mzize dakika 88.
Yanga ikacheza mchezo wa kimataifa wa hatua ya kwanza dhidi ya ASAS na bao la kwanza likifungwa dakika ya 22 na Azizi Ki na la pili la Kennedy Musonda dakika ya 52.
Kwenye upande wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga ilifungua pazia na KMC na kuichapa mabao 5-0. Kipindi cha kwanza kulifungwa bao moja tu dakika ya 17 na beki Dickson Job.
Mabao mengine yalifungwa kipindi cha pili na Aziz Ki dakika ya 59, Hafidh Konkoni (70), Mudathir Yahya (76) na Pacome Zouzoua (81).
Mchezo wa marudiano wa kimataifa dhidi ya ASAS, Yanga ilishidan 5-1, bao la kwanza likifungwa dakika ya saba na Max Nzengeli, huku mabao mengine yakifungwa na Hafidh Konkon (45), Pacome Zouazoua (55), Clement Mzize (69) na Max tena (90+).
Katika mechi ya pili ya Ligi Kuu, iliendeleza dozi kwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya JKT Tanzania. Bao la kwanza likifungwa na Aziz Ki dakika 45, huku mengine yakifungwa na Musonda (55), Yao Attohoula (64), Maxi dakika za 79 na 88.
Ukiangalia mtiririko huo, unaiona Yanga ikiwa tofauti zaidi katika upande wa mabao, licha ya kuwa na tabia kama ya msimu uliopita ilipokuwa chini ya Nesreddine Nabi, ya kufunga kipindi cha pili.
Wakatri wa Nabi, mabingwa hao wa Ligi Kuu walikuwa na uwezo wa kufunga kipindi cha pili, lakini idadi ya mabao haikuwa katika wingi wa sasa, ambao unachangiwa kwa kiasi kikubwa na kasi yao uwanjani.
Katika mahojiano baada ya mchezo dhidi ya JKT Tanzania, Kocha wa Yanga, Gamondi alikaririwa na gazeti hili akisema anataka kikosi chake kicheze kwa spidi na kwa kasi, hasa nusu ya pili ya mpinzani wakiwa huru kupishana na kutengezeana nafasi.
Kauli hiyo ni kama iliungwa mkono na kiungo, Khalid Aucho, ambaye alizungumza baada ya mchezo dhidi ya JKT Tanzania akiweka wazi kocha wao kuwapa uhuru wa kucheza, jambo linalowapa faida zaidi uwanjani.
"Kocha ametupa uhuru wa kucheza, lakini pia kuwa na spidi ambayo itawachosha wapinzani wetu na sisi ndiyo tutafanya vizuri," alisema Aucho.