Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ngoma: Mwamuzi ametunyima ubingwa

Kiungo wa Simba Fabrice Ngoma amesema kama siyo mwamuzi wa mchezo huo Dahane Beida basi walikuwa wanastahili kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Simba ilivaana na Berkane jana, kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar ambapo mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya bao 1-1 baada ya Simba kulala ugenini kwa mabao 2-0.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo huo, Ngoma ambaye ana uzoefu wa michuano hii ya kimataifa baada ya kucheza fainali mara kadhaa huko nyuma, alisema mwamuzi ndiye aliamua matokeo ya mchezo ule na hawakupewa nafasi ya kucheza muda unaotakiwa.

"Nafikiri mwamuzi aliimaliza ile mechi, tulijiandaa kikamilifu kwa ajili ya kuhakikisha kuwa tunapata ushindi kwenye mchezo ule na tunatwaa ubingwa.

"Hatukucheza muda unaotakiwa, nafikiri kama ni dakika nyingi sana basi tumecheza dakika 66 tu za muda wote kwenye mchezo huu.

"Maamuzi ya mwamuzi wa kati yaliathiri kwa kiasi kikubwa mchezo huu, lakini kwa ujumla tunapenda kuwapongeza Berkane kwa kutwaa ubingwa huo,' alisema Ngoma raia wa DR Congo.

Simba imepoteza ubingwa wa pili wa Shirikisho la Soka Afrika CAF baada ya mwaka 1993 kushindwa kushindwa kutwaa ubingwa wa Kombe la CAF baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Stella Abdjan ya Ivory Coast kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam baada ya suluhu ugenini.