Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Neville aiondoa Aston Villa nne bora EPL, aiweka Liverpool

Aston Villa ilichapwa mabao 2-0 na Wolves inayoshika mkia, matokeo yaliyoidondosha kutoka nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hadi nafasi ya nne. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Aston Villa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England (EPL) ikiwa na pointi 51 ilizokusanya katika michezo 28.

Beki wa zamani wa Manchester United, Gary Neville anaamini Aston Villa haitoweza kuwa miongoni mwa klabu zitakazomaliza katika nafasi nne za juu kwenye Ligi Kuu England (EPL) msimu huu.

Ijumaa iliyopita, Aston Villa ilichapwa mabao 2-0 na Wolves inayoshika mkia, matokeo yaliyoidondosha kutoka nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo hadi nafasi ya nne.

Akitoa maoni juu ya mwenendo wa EPL katika kipindi hiki ambacho inaelekea ukingoni, Neville amesema kuwa hadhani kama Aston Villa itapata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya akiamini haitomaliza katika nafasi nne za juu.

Badala yake, Neville ameitaja Liverpool akiiunganisha na Arsenal, Manchester City na Liverpool.

“Nadhani United (Manchester) itamaliza ikiwa ya tatu na siamini kama nasema hivyo kuanzia pale tulipokuwa wiki sita zilizopita.

“Hawana mvurugano, wana kitu kizuri kinachoendelea na kasi wako nayo. Timu zote zina mechi ngumu na zote zina changamoto mbele yao.

“Nadhani Liverpool itamaliza ya nne na nahisi Chelsea itamaliza ya tano. Nategemea Aston Villa katika nafasi tano za juu. Nilisema hilo kabla meneja wao ana uzoefu na mwenye hekima. Viungo wao walioumia wanawagharimu kiasi katika wiki za hivi karibuni,” amesema Neville.

Neville anaamini kama Aston Villa isingekumbwa na changamoto ya majeraha, ingekuwa na nafasi kubwa ya kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi.

Wachezaji wa nafasi ya kiungo wa Aston Villa ambao ni majeruhi kwa sasa ni Boubacar Kamara, John McGinn na Youri Tielemans.

Aston Villa kwa sasa inashika nafasi ya nne katika Ligi Kuu England ikiwa na pointi 51 wakati nafasi ya tano ipo Liverpool ikiwa na pointi 48.