Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MZEE WA FACT: Dharau za Carragher kwa AFCON ni muendelezo wa ukoloni

Mlinzi wa zamani klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya England, Jamie Carragher, ameonesha dharau kubwa kwa mashindano ya soka ya mataifa ya Afrika, AFCON.

Carragher ambaye sasa ni mchambuzi wa mpira kwenye luninga, alionesha dharau hiyo kwa AFCON kwa kusema mashindano hayo ni madogo na hayatambuliwi kama moja ya mashindano makubwa duniani.

Kauli hii ilikuja kutokana na mjadala wa Mohamed Salah kuwa na uwezekano au la, wa kushinda tuzo ya Ballon d’Or kutokana na kiwango chake cha mwaka huu hadi sasa.

Mjadala huo ulianza baada ya mechi ya ligi kuu England ambayo Liverpool ilishinda 2-0 dhidi ya Manchester City, Jumapili ya Februari 23.

Katika kuuchambua uwezo binafsi wa Mo Salah kwenye mechi hiyo na msimu huu kwa jumla, ndipo uliopoibuka mjadala wa kwamba raia huyo wa Misri anastahili kushinda Ballon d’Or au la.

Hapo ndipo Carragher alipoibuka na kusema Salah hawezi kushinda Ballon d’Or kwa sababu hana nafasi ya kutwaa taji lolote kubwa kwa kuwa anachezea timu ya taifa ya Misri ambayo haishiriki mashindano makubwa kwa kuwa AFCON ni mashindano madogo.

Akaongeza kwamba labda abahatike kushinda ligi ya mabingwa akiwa na klabu yake ya Liverpool ndiyo ataweza kuhesabiwa kama mchezaji aliyeshinda taji kubwa hivyo kuwa kwenye nafasi nzuri ya kushinda Ballon d’Or.

Ballon d’Or ni tuzo inayotolewa kwa kura kutoka kwa waandishi wa habari kutoka mataifa 100 duniani, na msimu uliopita ilichukuliwa na mchezaji wa klabu ya Manchester City na timu ya taifa ya Hispania, Rodri.

Wachezaji mbalimbali wa sasa na zamani kutoka Afrika wamemjia juu Carragher wakisema maneno yake ni ya kibaguzi na ni muendelezo wa fikra za kikoloni kwamba vitu vya Afrika ni duni na havina hadhi.

Kauli ya Carragher ilikuja siku tatu kabla ya kumbukumbu ya miaka 140 ya mkutano wa Berlin ambayo ndiyo chanzo kikuu cha dharau kwa Afrika kama aliyoionyesha Jamie Carrager.

Mkutano huo wa Berlin ndiyo uliofungua milango ya dharau, dhulma, unyanyasaji, uporaji mali na mateso kwa bara la Afrika na Waafrika wenyewe kwa ujumla kupitia ukoloni.

Mkutano huo uliofanyika kati ya Novemba 15, 1884 hadi Februari 26, 1885, uliitishwa na Kansela wa Ujerumani, Otto von Bismarck, na kuwakutanisha viongozi, mabalozi na wanadiplomasia kutoka mataifa mkubwa 14 duniani.

Lengo la mkutano huu lilikuwa kujadili na kukubaliana namna nzuri kwao ya kuligawa, kuligawana kulitawala bara la Afrika.

Sababu kubwa ya kuitishwa mkutano huu ni harufu ya hatari ambayo mataifa mkubwa waliiona mbele lao kwa wenyewe kwa wenyewe kuingia vitani kugombania mali za Afrika.

Kuepuka hilo, ndipo Kansela wa Ujerumani, Otto van Bismack, alipoitisha mkutano huu ili kuweka mambo sawa kupitia mazungumzo.

Miezi kadhaa kabla ya mkutano huu, maafisa wa Ufaransa walimuandikia barua Bismarck kuelezea hofu yao dhidi ya Uingereza namna anavyojimegea maeneo barani Afrika, hasa Misri na njia kuu ya biashara ya mfereji wa Suez.

Ujerumani pia ilikuwa na hofu na Uingereza kuhusu eneo lake iliyojimegea la Cameroon.

Ndipo Bismarck akaitisha mkutano huu na ajenda kuu ikawa kuchora ramani ya Afrika itakayoonesha nani anamiliki eneo gani baina yao.

Mataifa manne kati ya 14 yaliyohudhuria, yakiwemo Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na Ureno kama vinara kwa sababu tayari yalikuwa yameshajimegea maeneo mengi ya Afrika.

Mfalme wa Ubelgiji, Leopold, alituma wawakilishi wake ili mkutano umtambue kama mmiliki halali wa Congo kupitia kampuni yake ya “International Congo Society”, aliyoianzisha ili kuweka utawala wake kwenye bonde la mto Congo.

Zaidi ya hao, mataifa mengine tisa, mengi yao yalitoka mkutanoni bila kuambulia hata kipande kidogo cha ardhi ya Afrika.

Mataifa haya ni Austria, Hungary, Denmark, Urusi, Italia, Sweden-Norway, Hispania,  Uholanzi, Himaya ya Ottoman Empire (ambayo scheme yake kubwa sasa ni Uturuki), na Marekani.

Licha ya kwamba mkutano huu uliluhusu bara la Afrika, lakini hakuna nchi yoyote ya Afrika iliyoalikwa. Sultan wa Zanzibar aliomba kushiriki, lakini ombi lake likatupiliwa mbali.

Baada ya mkutano huu, Afrika ikagawanywa kama shamba la urithi kwa mataifa matano ya Uingereza, Ufaransa, Ureno, Ujerumani, Ubelgiji na Hispania.

Wakaja kuitawala Afrika na kupora mali za bara hili na kusababisha madhara mkubwa kwa watu wake ikiwemo umasikini mkubwa unaolisumbua bara hili hadi leo.

Ukoloni ulileta dharau, unyonge na fedheha kubwa kwa watu wa bara hili .

Japo sasa bara la Afrika ni huru na heshima kwa Waafrika inarudi, lakini kauli za watu kama Jamie Carragher zinakumbusha madhila ya mkutano wa Berlin, hasa zinapotoka katika mwezi ule ule ambao historia inaadhimisha miaka 140, tangu kufanyika wake.