Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ngorongoro, Serengeti zapewa wenyeji AFCON 2025

Muktasari:

  • Timu nne bora kwa maana ya zile zitakazoingia nusu fainali, zitakata tiketi ya moja kwa moja kushiriki michuano ya Kombe la Dunia U20 itakayochezwa Chile kuanzia Septemba 27 hadi Oktoba 19, 2025.

Timu za Taifa za Tanzania chini ya miaka 17, Serengeti Boys na ile ya chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, kila moja imepangwa kundi A na mwenyeji kwenye michuano ya AFCON kwa vijana itakayofanyika baadaye mwaka huu.

Serengeti Boys iliyofuzu michuano ya AFCON U17 itakayofanyika Morocco kuanzia Machi 30 hadi Aprili 19, 2025 ikishirikisha timu 16, imepangwa na wenyeji Morocco. Zingine ni Uganda na Zambia.

Kundi B kuna Burkina Faso, Afrika Kusini, Misri na timu moja itakayopatikana kutoka Ukanda wa Kisoka Afrika ya Kati (UNIFFAC 1).

Kundi C zipo Senegal, The Gambia, Somalia na Tunisia wakati Kundi D linaundwa na timu za Mali, Angola, Ivory Coast na timu nyingine itakayopatikana kutoka Ukanda wa Kisoka wa Afrika ya Kati (UNIFFAC 2).

Serengeti Boys inakwenda kushiriki michuano hiyo kwa mara ya tatu baada ya 2017 nchini Gabon na 2019 ilipofanyika hapa nchini lakini zote haikufanya vizuri.

Timu 10 bora katika michuano hiyo, zitafuzu Kombe la Dunia U-17 itakayofanyika Novemba mwaka huu nchini Qatar.

Kwa upande wa AFCON U20, Ngorongoro Heroes nayo imepangwa Kundi A na wenyeji Ivory Coast.

Michuano hiyo imepangwa kufanyika kuanzia Aprili 26 hadi Mei 18 mwaka huu nchini Ivory Coast ikishirikisha timu 13.

Mbali na Ngorongoro Heroes na Ivory Coast zilizopo kundi A, nyingine ni DR Congo, Ghana na Timu moja kutoka Ukanda wa Kisoka wa Afrika ya Kati (UNIFFAC 2).

Kundi B kuna Nigeria, Misri, Afrika Kusini na Morocco wakati Kundi C likiundwa na Senegal, Zambia, Kenya na Sierra Leone.

Hii ni mara ya pili Ngorongoro Heroes inashiriki michuano hiyo baada ya kufanya hivyo mwaka 2021 nchini Mauritania.

Timu nne bora kwa maana ya zile zitakazoingia nusu fainali, zitakata tiketi ya moja kwa moja kushiriki michuano ya Kombe la Dunia U20 itakayochezwa Chile kuanzia Septemba 27 hadi Oktoba 19, 2025.