Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwanasheria ataja kitakachomkuta Mwakinyo

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikielekeza bondia Hassan Mwakinyo kupelekewa wito wa kufika mahakamani kupitia gazeti la Mwananchi kufuatia kesi ya madai inayomkabili, wakili kiongozi wa kampuni ya uwakili ya Haki Kwanza, Alloyce Komba ameeleza kile kinachoweza kumpata kama ataendelea kutotokea mahakamani kusikiliza kesi.

Juzi, kesi hiyo ilitajwa mara ya kwanza na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Amiri Msumi aliyetoa uamuzi wa bondia huyo kupelekewa wito wa kufika mahakamani kupitia gazeti baada ya kukataa kupokea hati ya wito iliyowasilishwa kwake na msambaza nyaraka wa Mahakama.

Akizungumza kwa muktadha wa kisheria, Komba alisema Mwakinyo hawezi kukwepa kesi hiyo na kama ikitokea hatafika mahakamani, basi upande wa mashtaka utaomba isikilizwe upande mmoja na Mahakama haiwezi kukataa.

“Kupelekewa wito wa kufika mahakamani kupitia gazeti ni samansi mbadala, kama Mwakinyo atakwenda mahakamani Novemba 20, 2023 ili kusikiliza kesi yake itakapotajwa tena, basi itasikilizwa pande zote mbili na kujitetea.

“La sivyo  upande wa mdai ukiomba isikilizwe upande mmoja ikileta ushahidi wake (ex parte hearing) ikaamuriwa hivyo, Mwakinyo hatatafutwa tena, matokeo yake ni asubiri hukumu ya upande mmoja  (ex parte judgment) ambayo huwa na madhara makubwa.

“Mdai akishinda atapata decree (ya kukazia hukumu) anaweza kukamata akaunti za benki au mali zake mdaiwa,” alisema Komba akifafanua kwamba ili kesi isikilizwe pande zote ni upande wa Mwakinyo kufika.

Mwakinyo alifunguliwa kesi ya madai na kampuni ya PAF Promotion ikiwamo kuilipa Sh150 milioni ikiwa ni madhara ya jumla baada ya kutopanda ulingoni tofauti na mkataba aliosaini kwenye pambano la Septemba 29. Bondia huyo awali alidai sababu za kutopigana ni promota kukiuka makubaliano.

Wakili wa PAF Promotion, Herry Kauki alidai walipeleka wito Serikali ya mtaa, lakini Mwakinyo aligomea kupokea wito wa kufika mahakamani.