Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwanariadha mwingine wa Kenya afariki dunia

Muktasari:

  • Mwanariadha huyo amefariki dunia dakika chache baada ya kuvuka mstari wa kumaliza mbio ambapo alianguka ghafla.

Kenya. Mwanariadha wa Kenya, Charles Kipsang amefariki dunia katika mashindano ya mbio yaliyofanyikia nchini Cameroon.

Taarifa kutoka tovuti za Citizen Digital na The Star za Kenya, zinasema Kipsang amefariki baada ya kumaliza mbio hizo za milimani jana Jumamosi, Februari 24, 2024.
Inaelezwa Kipsang mwenye umri wa miaka 32, alikimbia hadi mwisho na alivuka mstari wa kumaliza huku akionekana amechoka ndipo alianguka ghafla na kufariki dakika chache baada ya kukimbizwa hospitalini.

"Mwanariadha huyo hakuwa na dalili zozote za afya mbaya, alianguka na juhudi za kumsaidia hazikuweza kufua dafu," imeeleza Citizen.

Chanzo cha kifo cha Kipsang bado hakijajulikana, lakini mamlaka za Cameroon zimeanzisha uchunguzi kubaini sababu.

Mbio hizo zilizopewa jina la Race of Hope, zinafanyikia katika eneo linalotajwa kuwa gumu hasa ambapo wanariadha hupanda na kushuka mlima huo uliopo zaidi ya mita 4,100 kutoka usawa wa bahari.

Kifo hicho kinaifanya Jumuiya ya riadha Kenya kuingia tena katika majonzi baada mwanariadha, Kelvin Kiptum aliyefariki dunia Februari 11, kuzikwa juzi Ijumaa ambayo ni siku moja kabla ya kifo cha Kipsang.

Ni wiki tatu zimepita baada ya Kiptum kufariki pamoja na kocha wake. Kiptum alifariki baada ya gari alilokuwa akiendesha kugonga mti katika barabara ya Eldama Ravine-Eldoret pamoja na kocha wake Gervais Hakizimana.

Kiptum alizikwa Ijumaa, katika mazishi ya kitaifa yaliyohudhuriwa na Rais wa Kenya, William Ruto.