Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwakinyo agomea pambano

Dar es Salaam. Bondia Hassan Mwakinyo ameweka wazi kuwa kesho hatoweza kupanda ulingoni kutokana na uongo na udanganyifu wa mapromota baada ya kubadilishiwa mpinzani Rayton Okwiri.

Mwakinyo amebainisha hayo kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram akiandika, “Binafsi, napenda sana kushukuru Mwenyezi Mungu kwa uzima na afya nilionayo leo, pia niwashukuru sana washabiki zangu kwa kujitokeza kwa nguvu kuonyesha shauku ya kunisapoti, nawashukuru sana Azam TV kwa kuendelea kutoa nafasi kwetu kama wachezaji wa ndani.

Naomba niweke hisia zangu wazi kwa mashabiki ya kuwa kesho sitaweza kupanda ulingoni kutokana na uongo na udanganyifu wa mapromota, binafsi sina tatizo na mtu ila pia naheshimu sana kazi yangu na siko tayari kuona watu wana nijaribu au kutaka kuharibu jina langu,"

Mwakinyo ametoa kauli hiyo leo Alhamis Septemba 28, 2023 baada kubadilishiwa mpinzani wa awali na kupewa bondia Julius Indongo wa Namibia.