Mwakinyo mambo yatibuka

JAHAZI la ubora wa Hassan Mwakinyo limezidi kuzama Afrika na kidunia ambako kote ameporomoka, tangu alipopigwa nchini England.
Nchini, Mwakinyo aliyekuwa namba moja kwenye kila uzani (pound for pound) tangu Oktoba 2018 ameshushwa na Tony Rashid ambaye sasa ndiye namba moja akiwa na nyota tatu na nusu, akimzidi nusu nyota Mwakinyo.
Ameporomoka pia Afrika ambako alikuwa kwenye 10 bora ya kila uzani, sasa ni wa 36, Tony akiwa wa 22.
Kwa mujibu wa mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia (Boxrec), kidunia katika uzani wake wa super welter, Mwakinyo ameporomoka kwa nafasi 21, ambako sasa ni wa 61 kutoka nafasi ya 40 aliyokuwepo wiki chache zilizopita.
Afrika, ni wanne, akiporomoka kwa nafasi mbili zaidi kwenye uzani wake unaoongozwa na Waafrika Kusini, Roarke Knapp na Brandon Thysse na Mcongo, Emmany Kalombo.