Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtanzania aweka historia michezo ya Olimpiki

Muktasari:

Michezo hiyo iliyohitimishwa jana, ilikuwa ikifanyika kwenye Mji wa Rio de Janeiro, Brazil.

Rio de Janeiro, Brazil. Kwa mara ya kwanza katika historia ya michezo ya Olimpiki tangu mwaka 1980 baada ya Suleiman Nyambui na Filbert Bayi kufanya vizuri Moscow, Mtanzania Alphonce Simbu jana aliweka historia baada ya kushika nafasi ya tano katika mbio za marathon  za kilometa 42.

Michezo hiyo iliyohitimishwa jana, ilikuwa ikifanyika kwenye Mji wa Rio de Janeiro, Brazil.

Katika mbio hizo zilizoanza mchana, Simbu angalau alionyesha tumaini jipya katika michezo ya Tanzania licha ya kukosa medali kwa kuonyesha bidii tangu mwanzo huku akiwaacha wanariadha zaidi ya 155 walioshiriki mbio hizo.

Simbu na wanariadha wengine wa Tanzania, Said Makula na Fabian Joseph ndio waliokuwa tegemeo la mwisho katika michezo hiyo baada ya wanamichezo wengine kutolewa hatua za awali. Makula alishika nafasi ya 43 wakati Fabian nafasi ya 112.