Msigwa: Weledi utatuweka pazuri

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa akimwakilisha waziri, Damas Ndumbaro katika mkutano mkuu wa mwaka wa Yanga 2024, amesisitiza juu ya weledi katika namna ya uendeshaji kwa klabu za Ligi Kuu Bara.
Msigwa amesema hayo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam wakati akiwapongeza viongozi Yanga kwa mageuzi makubwa ambayo wameyafanya.
"Kwa niaba ya Waziri naomba kuwafikishia salamu kwa kuwapongeza kwa ubingwa wa 30, amewapongeza pia kwa ubingwa wa FA, ameniambia niwaambie yupo pamoja nanyi," amesema Msigwa na kuongeza;
"Kwa dhati ya moyo wangu naomba kuwapongeza kwa mafanikio makubwa, upande wa wizara kwa niaba ya Serikali jambo muhimu ni namna Yanga mmetengeza weledi katika uendeshaji. Serikali tunatamani kuona klabu zikiwa na uendeshaji mzuri wa uendeshaji. Tunataka kywa sehemu ya mafanikio na sio usuluhishi wa migogoro. Naiona Sayansi kwenye klabu ya Yanga."
Msigwa alimalizia kwa kuwataka Yanga kuendelea kuwa mfano mzuri juu ya namna ya uendeshaji wa klabu; "Kuna mahali mmesogea, natamani kuona klabu za Tanzania ifike hatua ziwe kiuendeshaji sawa na klabu kubwa za soka Ulaya."