Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Moalin arejeshwa Yanga kumsaidia Pedro Goncalves

Klabu ya Yanga imemrejesha, Abdihamid Moalin kuwa kocha Msaidizi chini ya Kocha Mkuu Pedro Gonçalves.

Muktasari:

  • Kocha Abdihamid Moalin amewahi kuhudumu Yanga kwa nyakati tofauti akiwa Kocha Msaidizi na Mkurugenzi wa Ufundi.

Yanga imetangaza kumrudisha kikosini Abdihamid Moalin kuwa Kocha Msaidizi wa kikosi chao cha wakubwa kinachonolewa na Kocha Mkuu Pedro Goncalves.

Uamuzi huo umefanywa leo Jumatatu, Machi 23, 2026 baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo.

Taarifa ambayo imetolewa na klabu hiyo, imefafanua kwamba licha ya changamoto kadhaa ambazo inapitia zinazochangia isiwe na mwenendo mzuri kwa siku za hivi karibuni, udhaifu wa kiufundi pia ni sababu mojawapo.

“Aidha, licha ya changamoto hizo, Uongozi umegundua uwepo wa changamoto ya kiufundi inayoifanya Timu icheze aina tofauti ya uchezaji (style of play), na ile ambayo imezoelekea na kuendana na wachezaji walio ndani ya kikosi.

“Changamoto hii ya kiufundi imekuwa sababu ya kuifanya timu kupata wakati mgumu kupata matokeo mazuri na kucheza vizuri pia kwenye baadhi ya michezo ya Ligi Kuu.

“Hivyo, katika kuitatua changamoto hii, Uongozi wa Young Africans Sports Club umefikia uamuzi wa kumuongeza kwenye benchi la Ufundi, Kocha Abdihamid Moalin kama Kocha Msaidizi wa Kocha Pedro Goncalves.

“Kocha Moalin amewahi kuhudumu katika Klabu yetu kama Mkurugenzi wa Ufundi na Kocha Msaidizi katika vipindi tofauti chini ya Kocha Sead Ramovic na Miloud Hamdi na kupata mafanikio makubwa ya kushinda Kombe la Ligi Kuu 2024/2025, Kombe la Shirikisho la CRDB 2025na Kombe la Muungano 2025. Uongozi wa Young Africans SC unamkaribisha Kocha Moalin na kumtakiwa kila la kheri kwenye majukumu yake mapya kwa kushirikiana na Makocha wengine ndani ya kikosi chetu,” imefafanua taarifa ya Yanga.

Yanga pia imetaja changamoto ya majeraha kwa idadi kubwa ya wachezaji wake kama sababu nyingine ambayo imewaathiri.

Katika mechi tatu zilizopita za Ligi Kuu ya NBC, Yanga imepata matokeo ya sare ambapo mechi mbili imetoka bila kufungana ambazo ni dhidi ya Azam FC na TRA United na mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar imepata sare ya bao 1-1.