Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mo Dewji anavyotesa na utajiri Afrika, Dangote kinara

Muktasari:

  • Uwekezaji katika viwanda vya nguo, unga wa ngano na sembe, mafuta ya kupikia, sabuni, sukari na vinywaji unatajwa kama miongoni mwa vyanzo vya utajiri huo wa Dewji.

Dar es Salaam. Mwekezaji wa Simba na Mfanyabishara Mohammed Dewji anaufunga mwaka 2025 kibabe kwa kubakia katika nafasi ya 12 katika orodha ya Forbes ya mabilionea Afrika.

Katika orodha ya Forbes ya Desemba 8, 2025 ya Mabilionea wa Afrika, Dewji amelinda utajiri wake wa Dola 2.2 bilioni (Sh5.8 trilioni) ambao alikuwa nao katika orodha ya Forbes iliyotolewa Machi 29, mwaka huu akiwa katika nafasi hiyohiyo ya 12.

Dewji pia anaendelea kuwa bilionea mwenye umri mdogo zaidi Afrika kwa mujibu wa chati hiyo ya Forbes lakini pia ndiye anayeongoza kwa utajiri katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Uwekezaji katika viwanda vya nguo, unga wa ngano na sembe, mafuta ya kupikia, sabuni, sukari na vinywaji unatajwa kama miongoni mwa vyanzo vya utajiri huo wa Dewji.

Orodha hiyo imetawaliwa zaidi na mabilionea kutoka nchi za Nigeria, Afrika Kusini na Misri.

Mnigeria Aliko Dangote aliyeongeza utajiri wake kutoka Dola 23.9 bilioni aliokuwa nao mwezi Machi, 2025 hadi Dola 25.6 bilioni mwezi huu, anaongoza chati ya mabilionea Afrika.

Ifahamike, Dangote ambaye ameonekana kuwekeza zaidi katika uzalishaji wa saluni na sekta ya nishati, ameongoza chati ya Mabilionea Afrika kwa miaka 14 mfululizo.

Johann Rupert mwenye utajiri wa Dola 16.2 bilioni anashika nafasi ya pili katika orodha hiyo na nafasi ya tatu inashikwa na Nicky Oppenheimer mwenye utajiri wa Dola 10.5 bilioni.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Patrice Motsepe anashika nafasi ya 10 katika orodha hiyo akiwa na utajiri unaokadiriwa kufikia Dola 3.6 bilioni.


ORODHA YA MABILIONEA 10 AFRIKA 2025

1. Aliko Dangote- Dola 25.6 bilioni

2. Johann Rupert- Dola 16.2 bilioni

3. Nicky Oppenheimer- Dola 10.5 bilioni

4. Nassef Sawiris- Dola 8.4 bilioni

5. Mike Adenuga- Dola 6.3 bilioni

6. Abdulsamad Rabiu- Dola 8.5 bilioni

7. Naguib Sawiris- Dola 5 bilioni

8. Koos Bekker- Dola 3.8 bilioni

9. Patrice Motsepe- Dola 3.6 bilioni

10. Mohamed Mansour- Dola 3.4 bilioni