Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Missiru wa DRFA afungiwa miaka sita na TFF

Ramadhan Missiru, Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA).

Muktasari:

  • Adhabu hizi zinaakisi dhamira ya TFF kuhakikisha nidhamu, uwajibikaji na utii wa sheria vinaendelea kupewa kipaumbele katika uendeshaji wa michezo nchini.
no

Dar es Salaam. Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imemfungia Ramadhan Missiru, Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), kutojihusisha na shughuli zozote za mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka sita.

Missiru alipatikana na hatia ya makosa mawili ya ukiukwaji wa maadili yaliyobainishwa na kamati hiyo katika kikao chake kilichofanyika Mei 8, 2025 jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya TFF iliyotolewa leo Mei 13, 2025 na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Clifford Ndimbo, Missiru alishtakiwa na Sekretarieti ya TFF kwa makosa mawili ikiwemo kushindwa kutii maamuzi ya Kamati ya Maadili, kinyume na Kanuni ya 73(8) ya Maadili ya TFF Toleo la 2021. Kosa lingine ni kuchochea umma, kinyume na Kanuni ya 73(4) ya Maadili ya TFF Toleo la 2021.

Baada ya kupitia ushahidi uliowasilishwa na pande zote, Kamati ya Maadili ilibaini kuwa Missiru alitenda makosa hayo na hivyo ikamfungia kutoshiriki shughuli za mpira wa miguu kwa miaka sita kuanzia Mei 8, 2025 huku akitozwa faini ya Sh5 milioni.

Katika kikao hicho hicho, Kamati ya Maadili pia ilisikiliza shauri dhidi ya Thabit Zakaria, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Azam, aliyeshtakiwa kwa kosa la kuchochea umma kinyume na kanuni ya 73(4). Hata hivyo, baada ya kupitia ushahidi uliowasilishwa, kamati ilibaini kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha kumtia hatiani, hivyo Zakaria hakukutwa na hatia dhidi ya kosa aliloshtakiwa nalo.

Adhabu hizi zinaakisi dhamira ya TFF kuhakikisha nidhamu, uwajibikaji na utii wa sheria vinaendelea kupewa kipaumbele katika uendeshaji wa michezo nchini.