Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbappe na mabao 44 Ligi ya Mabingwa Ulaya

Muktasari:

  • Mbappe raia wa Ufaransa amekuwa na ubora wa hali ya juu kwenye michuano mbalimbali na juzi aliwaonyesha mashabiki wa timu hiyo kuwa anaweza kuipa ubingwa huo baada ya kufunga bao la kwanza na kufikisha mabao 44 kwenye Ligi ya Mabingwa, huku bao lingine la timu hiyo likifungwa na Bradley Barcola likiwa ni la kwanza kwake kwenye michuano hiyo.

Paris, Ufaransa. PSG imeanza vizuri mchezo wake wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuichapa Real Sociedad mabao 2-O, huku staa wa timu hiyo, Kylian Mbappe akiweka rekodi mpya kwenye michuano hiyo.

Mbappe raia wa Ufaransa amekuwa na ubora wa hali ya juu kwenye michuano mbalimbali na juzi aliwaonyesha mashabiki wa timu hiyo kuwa anaweza kuipa ubingwa huo baada ya kufunga bao la kwanza na kufikisha mabao 44 kwenye Ligi ya Mabingwa, huku bao lingine la timu hiyo likifungwa na Bradley Barcola likiwa ni la kwanza kwake kwenye michuano hiyo.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Parc Des Princes nchini Ufaransa, Real Sociedad ilionyesha kiwango kizuri dakika 45 za kwanza, lakini juhudi zao hazikuzaa matunda.

Pamoja na kwamba tetesi zimekuwa zikisema kuwa Mbappe anaweza kujiunga na Real Madrid mwishoni mwa msimu huu, staa huyo bado ameendelea kuonyesha makali yake kwenye timu hiyo sasa anadaiwa mabao 96 ili aweze kukaa kileleni kwenye chati ya ufungaji ambayo inaongozwa na Cristiano Ronaldo aliyefunga mabao 140.

Juu ya Mbappe yupo staa wa Bayern Munich, Thomas Muller mwenye mabao 53 na Roberto Lewandowiski wa Barcelona mwenye mabao 92 ambao ndio wanaocheza soka la ushindani.
Mbappe mwenye miaka 25 mabao hayo 44 sasa yanamfanya alingane na Mohammed Salah wa Liverpool.

Hivi karibuni mshindi huyo wa Kombe la Dunia, ambaye alijiunga na PSG mwaka 2017, alisema furaha yake ni kuona siku moja anatwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na jezi ya PSG.

Hata hivyo, pamoja na ushindi huo, bado PSG itatakiwa kufanya kazi ya ziada kwenye mchezo wa pili Machi 5 nchini Hispania, kutokana na ubora wa Real Sociedad ambao wameuonyesha kwenye mchezo huu wa kwanza.


Vinara wa mabao Ligi ya Mabingwa Ulaya

Cristino Ronaldo    140
Lionel Messi        129
Robert Lewandowski   92
Karim Benzema       90
Raul Gonzalez       71
Ruud Van Nistelrooy 56
Thomas Muller       53
Thiery Henry        50
Alfred di Stefano   49
Andriy Shevchenk0   48
Eusebio             46
Filippo Inzaghi     46
Kylian Mbappe       44
Mohammed Salah      44