Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabao ya Mbappe yaiweka pazuri PSG

Mshambuliaji kinda Kylian Mbappe amekuwa mchezaji wa kwanza mwenye umri mdogo kufikisha mabao 50 katika Ligi Kuu Ufaransa.

Mbappe anayecheza Paris Saint Germain (PSG) alifunga mabao mawili katika ushindi ambao timu hiyo ilishinda 3-0 dhidi ya Nimes.

Bao jingine la mabingwa hao wa Ligi Kuu Ufaransa, lilifungwa na Christopher Nkunku.

Pia katika mchezo mwingine uliochezwa juzi, Amiens ikiwa nyumbani ilivuna pointi tatu baada ya kuigagadua Nice bao 1-0.

Kocha wa PSG Thomas Tuchel ameiweka timu hiyo katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa msimu huu.

Mshambuliaji huyo aliyefikisha umri wa miaka 20, miezi miwili na siku nne, amevunja rekodi iliyokuwa ikishikwa na Yannick Stopyra aliyoweka mwaka 1982.

Licha ya kutokuwepo mshambuliaji nyota Neymar, PSG imeendelea kupata matokeo mazuri katika mashindano mbalimbali msimu huu.

Hivi karibuni iliichapa Manchester United mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Neymar atakuwa nje ya uwanja wiki saba akikabiliwa na majeraha ya kifundo cha mguu alichofanyiwa upasuaji. Mbappe kwasasa ndiye tegemeo la PSG katika kikosi hicho na mabao yake yamekuwa yakiiweka timu hiyo katika nafasi nzuri katika ligi ya ndani na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

PSG imeendelea kubaki kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 68 baada ya kushinda mechi 22 katika michezo 25 iliyocheza.

Wakati PSG ikiongoza, Amiens inashika nafasi ya 16 katika msimamo ikiwa na pointi 36 katika mechi 26 ilizocheza.