Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ACT-Wazalendo yajizatiti kupigania Liganga-Mchuchuma

Muktasari:

  • Chama hicho kimesisitiza kuwa hakitachoka kuupigania m mradi huo uanze kwa sababu una faida na manufaa yatakayowanufaisha wananchi wa Ruvuma, Njombe wanufaike na utajiri wa madini hayo sambamba na migodi iliyopo katika mikoa hiyo.

Songea. Chama cha ACT- Wazalendo kimesema kitaendelea kuuvalia njuga suala la Liganga na Mchuchuma ambao ni mradi wa kimkakati unaolenga kukuza uchumi wa viwanda kwa kuanzisha sekta za msingi zitakazosaidia sekta nyingine katika mnyororo wa thamani.

Kimesisitiza hakitachoka kuupigania  mradi huo uanze kwa sababu una faida na manufaa yatakayowanufaisha wananchi wa Ruvuma, Njombe wanufaike na utajiri wa madini hayo sambamba na migodi iliyopo katika mikoa hiyo.

Mapema mwaka huu, Waziri wa Viwanda, Dk Selemani Jafo alinukuliwa akisema Serikali ipo katika hatua za mwisho za kimkataba za utekelezaji wa mradi huo.

Mradi huo unakadiriwa kuzalisha mapato ya dola za Marekani 1.2 kila mwaka ambazo karibu na Sh 1.3 trilioni kutokana na uzalishaji wa madini ya chuma, titani, vanadium na salfuti ya Alumini.

Kiongozi mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amebainisha hayo jana Jumatatu Julai 7, 2025 akihutubia wananchi wa eneo Soko Kuu Songea Mjini mkoani Ruvuma katika mwendelezo ziara ya operesheni 'Majimaji Linda Kura' yenye lengo la kuhamasisha Watanzania kushiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba ili kurejesha thamani ya kura zao.

Katika hotuba yake, Zitto amesema:"ACT- Wazalendo tunataka mradi wa Liganga na Mchuchuma uanze mara moja na tutahakikisha unaanza kwa sababu faida yake ni kubwa mno."

"Tunataka kuona wananchi wa halmashauri mbalimbali wana miliki hisa katika uzalishaji na sikupewa zawadi zawadi za ujirani mwema au za kurudisha mchango kwa jamii," amesema Zitto ambaye amewahi kuwa mbunge wa Kigoma Mjini.

Amesema akiwa bungeni kila akisimama amekuwa akililia utekelezaji wa mradi wa Liganga na Mchuchuma lakini hadi sasa bado haujaanza kufanya kazi ili kuleta unafuu wa upatikanaji wa chuma nchini na kupunguza uagizaji wa bidhaa hiyo nje ya nchi.

"Tanzania inao utajiri wa chuma ambacho kinaweza kutumika kwa miaka zaidi ya 200 na bado kikabaki lakini yamekosekana maarifa. Ajira za vijana hakuna, hakuna kwa sababu bidhaa za msingi za viwandani zinatokana na chuma ambacho bila makaa ya mawe huwezi kukiyeyusha," ameeleza.

Amedai tangu aondoke bungeni mwaka 2020 uchangiaji wa wabunge unaolenga kuishikiniza Serikali kutekeleza  mradi wa Liganga na Mchuchuma sambamba makaa ya mawe yanayopatikana mkoani Ruvuma umekuwa wa kusuasua.

"Lini umemsikia mbunge anazungumzia kuhusu makaa ya mawe au lini umewasikia wabunge wa Wilaya ya Mbinga zote wanazungumzia makaa ya mawe ambayo yanachimbwa wilayani humo.

"Hivi wanajali namna ambavyo malori ya makaa ya mawe yanavyoharibu barabara? Au wanajali namna malori ya makaa ya mawe yanavyopinduka na kumwaga makaa ya mawe yanayoathiri afya za wananchi kutokana na vumbi? Hawajali," amedai Zitto.

Kutokana na hilo, Zitto amesema ndio maana ACT Wazalendo imeamua kushiriki uchaguzi ili kupambana hadi dakika za mwisho ili kutatua changamoto zinazowakabili Watanzania wa maeneo mbalimbali.

"Hatua ya kwanza ni kuiondoa CCM ili kutekeleza sera mbadala, tukiendelea hivi maana hivi na kuwasikiliza watu wanaotaka tususie uchaguzi tutakuwa tumesalimu amri kwa watu ambao hawawezi kujiongeza hata kidogo," amesema Zitto.

Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa ACT Wazalendo mkoa wa kichama Selous, Abdallah Mtutura amesema chama hicho kimeamua kuchukua nafasi ya kuwatatetea Watanzania ili kujua haki zao msingi.

Mwenyekiti wa Mkoa wa Kigoma, Kiiza Mayeye amesema kama kuna wakati unaofaa kuwaweka watu madarakani, kinachohitajika ushirikiano wa kukiondoa chama hicho tawala.

Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake ACT- Wazalendo, Janeth Rithe amesema hicho kitateua wagombea watakaotetea masilahi ya Watanzania, akiwaomba wananchi kuwaubga mkono katika uchaguzi mkuu.