Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Matatizo ya Liverpool yananihusu

Muktasari:

  • Ushindi huo wa mabap 3-0 uliwezeshwa na mabao ya Murillo, Nicolo Savona na Morgan Gibbs-White aliyepigilia jiwe la mwisho dakika ya 78.

London, England. Kocha wa Liverpool, Arne Slot amesema yeye ndio anapaswa kupewa lawama kutokana na mfululizo mbaya wa matokeo ambayo timu hiyo imekuwa ikiyapata tangu kuanza kwa msimu huu.

Wikiendi iliyopita, Nottingham Forest ilipata ushindi mkubwa zaidi chini ya Sean Dyche ambaye amechukua mikoba hivi karibuni.

Ushindi huo wa mabap 3-0 uliwezeshwa na mabao ya Murillo, Nicolo Savona na Morgan Gibbs-White aliyepigilia jiwe la mwisho dakika ya 78.

Huo ulikuwa ni mchezo wa nane kwa Liverpool kupoteza kati ya 11 za michuano yote msimu huu na sasa imetupwa hadi nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi.

Akizungumza baada ya mechi, Slot alisema:"Nataka kusema kwamba mimi ndiye ninayepaswa kuwajibika kwa vipigo hivi tunavyopata. Unaposhinda unawajibika, na unapopoteza pia unawajibika. Siwezi kutoa visingizio kwa matokeo tunayopata.  Ni jukumu langu kuwajibika pale timu inaposhinda au kupoteza."

"Kikubwa ninachokiona katika timu bado kuna ushirikiano, mashabiki weti walibaki hadi mwisho wa mchezo licha ya kuongozwa kwa muda mwingi, haikuwa hivyo dhidi ya Manchester City (wiki mbili zilizopita),"alisema Slot na kuongeza kuwa katika mechi ya Forest aliona utofauti mkubwa kwa wachezaji wake ambapo walau walitengeneza nafasi nyingi.

"Hivi karibuni, mara kwa mara, tumekuwa tukikosa nafasi za kufunga mabao kisha tunaruhusu sisi, hilo haliwezi kuendelea msimu mzima, tunahitaji kufunga mabao, ukiwa unatawala mechi na kufunga bao moja mpinzani hupoteza morali. Lakini kilichotokea katika mechi hii ni kinyume… wao walipata morali kubwa baada ya kufunga bao la kwanza."

Alipoulizwa juu ya utata wa bao la kwanza la Forest, Slot bado aliendelea kusisitiza kwamba hakuna kisingizio chochote kwa sasa badala yake yeye ndio anatakiwa alaumiwe.

Liverpool itakuwa mwenyeji wa PSV ya Uholanzi wiki hii katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na baada ya hapo itakutana na West Ham Jumapili ya  wikiendi ijayo kabla ya kuwa na kibarua kigumu dhidi ya Sunderland.