Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United, Tottenham kusaka rekodi Ulaya

Muktasari:

  • Mara ya mwisho timu za England kukutana katika fainali ilikuwa ni Mei 29, 2019 ambapo Chelsea ilikutana na Arsenal katika fainali hizi huku Tottenham ikikutana na Liverpool kwenye mashindano ya UEFA.

Manchester, Engalnd. Manchester United leo itashuka dimbani kukabiliana na Athletic Bilbao katika mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya UEFA Europa League utakaochezwa kwenye Uwanja wa Old Trafford, jijini Manchester.

United inaingia kwenye mchezo huo wakiwa kifua mbele baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 ugenini wiki iliyopita, ushindi uliowapa nafasi kubwa ya kutinga fainali ya mashindano hayo.

Katika mchezo huo wa kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa San Mamés, mabao ya United yalifungwa na Casemiro pamoja na nahodha Bruno Fernandes aliyefunga mawili, likiwemo moja kwa mkwaju wa penalti. Bilbao walikamilisha mchezo huo wakiwa pungufu baada ya beki, Dani Vivian kuonyeshwa kadi nyekundu.

Kwa upande wa Athletic Bilbao, wanahitaji ushindi wa zaidi ya mabao matatu bila kuruhusu ili kuibuka na tiketi ya fainali, jambo ambalo linaonekana kuwa gumu kutokana na mazingira ya ugenini na kiwango cha wapinzani wao katika mashindano hayo.

Pamoja na faida waliyonayo Man United hawana sababu ya kulizika na matokeo kwani historia ya michuano ya Ulaya imejaa matukio ya timu kupindua matokeo. Ikiwa Bilbao watafanikiwa kufunga bao mapema, shinikizo linaweza kuongezeka kwa wenyeji. Hivyo nidhamu ya ulinzi inatakiwa kuwa kubwa kwa United.

United ambayo ilikuwa haipewi nafasi kubwa ya kufika mbali kwenye mashindano haya, iliwashangaza wengi baada ya kupindua matokeo katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Lyon kwenye Uwanja wa Old Trafford. Pengine kutokana na kufanya vibaya kwenye Ligi Kuu ya England, huwenda United wamelenga kuwa mabingwa katika mashindano haya ili kurudi kwenye mashindano ya Ulaya msimu ujao.

Mchezo mwingine wa nusu fainali ya Kombe la Europa utafanyika kwenye Uwanja wa Aspmyra, Norway ambapo Bodo/Glimt watakuwa nyumbani kuikaribisha Tottenham ambayo itaingia ikiwa na mtaji wa mabao 3-1 iliyopata katika mchezo wa kwanza uliofanyika England.

Huenda ikashuhudiwa tena timu mbili za England kukutana katika fainali hizi iwapo Man United na Tottenham zitafanikiwa kufuzu katika hatua ya fainali kwani mara ya mwisho ilikuwa ni Mei 29, 2019 ambapo Chelsea ilikutana na Arsenal katika fainali hizi huku Tottenham ikikutana na Liverpool kwenye mashindano ya UEFA.

Mshindi wa jumla kati ya Tottenham au Bodo/Glimt atakutana na mshindi wa jumla kati ya Man United au Athletic Bilbao ambapo mchezo wa fainali utafanyika Mei 21 mwaka huu kwenye Uwanja wa San Mamés, Bilbao, Hispania.