Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo matano muhimu Siku ya Mwananchi, Dk Mpango ndani

Mashabiki wa Yanga wakiwa katika foleni ya kuchukua supu, ikiwa ni miongoni mwa shughuli zinazofanywa na klabu hiyo kuelekea kilele cha siku ya mwananchi. Picha na Yanga

Dar es Salaam. Siku iliyongojewa kwa hamu na mashabiki, wanachama na wapenzi wa Yanga ya utambulisho wa kikosi chao cha msimu ujao imefika ambayo ni leo na macho, masikio na hisia zote zitaelekezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa ambako jambo hilo linafanyika.

Ni kilele kinachihitimisha awamu ya sita ya tamasha hilo ambalo kwa mara ya kwanza lilifanyika 2019 likiwa maalumu kwa ajili ya kuonyesha kikosi cha timu hiyo katika msimu unaofuata lakini kushiriki huduma za kijamii kama vile kusaidia makundi maalumu, kuchangia damu na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali.


Makamu wa rais ndani

Kwa mara ya kwanza mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais Tanzania, Dk Philip Mpango ambaye leo Jumapili Agosti 4, 2024 amesafiri kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam kwa kutumia Usafiri wa Treni ya Kisasa ya Umeme inayotumia Reli ya Kisasa (SGR) akiwa na na mwenza wake, Mama Mbonimpaye Mpango.


Makombe uwanjani

Mbali na hilo, mashabiki wa Yanga na wapenda soka ambao leo watajitokeza katika Uwanja wa Benjamin Mkapa watakuwa na fursa ya kuona makombe yaliyochukuliwa msimu uliopita ambayo ni Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la CRDB pamoja na Kombe la Toyota ambalo wamelitwaa hivi karibuni huko Afrika Kusini ambako walialikwa.

Baada ya kucheza na Kariobang Sharks, Aigle Noir, Zanaco, Vipers na Kaizer Chiefs katika mechi za matamasha yaliyopita, Yanga leo itakabiliana na bingwa wa Zambia na Kombe la Kagame, Red Arrows.

Mchezo wa Yanga dhidi ya Arrows umepangwa kuanza saa 2:00 usiku ambapo mashabiki wa Mabingwa hao wa Tanzania, watakiona kwa mara ya kwanza kikosi chao cha msimu ujao kikicheza dimba la Mkapa.

Hapana shaka hamu kubwa ya Wanayanga ni kuwaona mubashara nyota wao saba ambao wamesajiliwa katika dirisha kubwa la usajili linaloendelea ambao kuna uwezekano mkubwa wakatambulishwa na msemaji wa timu hiyo, Haji Manara.

Baada ya kukosa tamasha moja lililopita kutokana na kutumikia adhabu ya kifungo alichopewa na TFF, Haji Manara anarudi kazini kunogesha tamasha hilo ikielezwa amejiandaa vilivyo kuhakikisha anafanya utambulisho wa kibabe kwa mastaa wa kikosi hicho.

Abubakar Khomeny, beki Chadrack Boka, viungo, Clatous Chama, Duke Abuya,Aziz Adambwile na washambuliaji Jean Baleke na Prince Dube.


Burudani imesheheni

Kundi kubwa la wasanii linatarajiwa kutumbuiza katika kilele cha Wiki ya Mwananchi leo likiongozwa na Harmonize.

Ukiachana na Harmonize wasanii wengine waliothibitishwa kuburudisha ni pamoja na Christian Bella, Marioo,Chobis Twins,Pado,Billnas, Sir Jay na Meja Kunta.

Ukiacha wanamuziki hao pia Dj Ally B kama kawaida ataendelea kuwapa burudani ya kuimba na kupiga muziki kama ilivyokuwa matamasha yaliyopita.


Wachezaji kung'arishwa

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema timu hiyo mara itapoingia itakuwa kwenye vazi maalumu nje ya suti mlizozoea na baada ya hapo itaingia uwanjani kusalimia mashabiki kwa kuzunguka ikiwa na mavazi mengine.

Haitaishia hapo, timu hiyo itakapoingia kujaribu uwanja itakuwa kwenye vazi lingine na baadaye kuvaa vazi lingine wakati wa kupasha misuli.

Hata itakapocheza mechi itavaa jezi za nyumbani kwenye kipindi cha kwanza lakini kipindi cha pili itavaa uzi wa ugenini zikiwa zote ni za msimu ujao.


Maandalizi ya kasi

Pale Benjamin Mkapa jana kulikuwa na tamasha la Simba Day lakini Yanga ilishakuwa imejipanga sawasawa kuhakikisha hakuna kinachoharibu mpango wao kuelekea kilele Cha wiki ya Wananchi.

Saa sita usiku wa kuamkia Leo Yanga ilivamia uwanjani hapo baada ya kuweka kila kitu chao jana mapema Uwanja wa Uhuru na kazi ya kuupamba kwa haraka uwanja huo ikaanza kwa kikosi kazi cha watu wasiopungua 150 hadi leo asubuhi.

Kikosi kazi hicho kimepewa masharti mawili tu kuhakikisha uwanja huo unapendeza kwa rangi za Yanga lakini pia kusionekane mapambo yoyote ya watani wao Simba kwenye uwanja huo.


Mashabiki kazi kwao

Ikumbukwe kwamba tiketi za kutazama mchezo huo zilimalizika mapema juzi Ijumaa na zoezi la uuzaji lilifungwa rasmi, hivyo kazi leo ni kwa mashabiki kwenda kukitazama kikosi chao.