Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Luis Díaz ataka kuondoka Liverpool

Muktasari:

  • Díaz mwenyewe anasemekana kuwa anataka kujaribu changamoto mpya lakini Anfield imeweka ugumu wa kumuachia nyota huyo.

Winga wa Liverpool, Luis Díaz, ameripotiwa kuwasilisha ombi la kutaka kuondoka Anfield msimu huu wa joto, huku Bayern Munich wakikumbana na pigo baada ya kukataliwa ofa yao ya pauni milioni 58.6 sawa na shilingi za Kitanzania 193.4 bilioni.

Kwa mujibu wa The Athletic, Bayern Munich waliwasilisha ofa hiyo Jumanne iliyopita, lakini Liverpool waliikataa mara moja. Klabu hiyo ya Anfield imeweka wazi kuwa haijapanga kumuuza nyota huyo wa Colombia licha ya mvutano unaoendelea.

Liverpool: Hatumuzi!

Ripoti zinasema kuwa Liverpool wanamtathmini Díaz kwa zaidi ya pauni milioni 86 (Sh283 bilioni), ingawa dau hilo kubwa linaaminika kuwa la kimahesabu tu si bei halisi ya soko. Hata hivyo, msimamo wao uko wazi wakikazia kuwa mchezaji hawezi kuuzwa msimu huu.


Historia fupi ya mchezaji

Díaz alijiunga na Liverpool kutoka FC Porto Januari 2022 kwa ada ya awali ya pauni milioni 37.5 (Sh123 bilioni), na hadi sasa ameshacheza mechi 148 na kufunga mabao 41 kwa klabu hiyo.

Msimu uliopita, alitoa mchango mkubwa kwenye kikosi cha kocha mpya Arne Slot, akianza mechi 28 za Premier League, akifunga mabao 13 na kutoa pasi saba za mabao akisaidia Liverpool kutwaa taji la Ligi Kuu England kwa mara ya kwanza tangu 2020.


Bayern waendelea kushindwa kuwapata nyota

Kukwama kwa dili la Díaz kunakuja baada ya Bayern kupoteza pia fursa ya kuwasajili nyota wawili muhimu: Florian Wirtz, ambaye alichagua Liverpool badala ya Bayern akisajiliwa kwa mkataba wa pauni milioni 118 (Sh400 bilioni). Mwingine ni Nico Williams wa Athletic Club, ambaye aliamua kusaini mkataba mpya badala ya kuhamia Bavaria au Barcelona.

Díaz ataondoka?

Pamoja na ofa hiyo ya Bayern na tetesi kuhusu nia ya Barcelona, bado haijafahamika wazi iwapo Liverpool watabadilisha msimamo wao. Díaz mwenyewe anasemekana kuwa anataka kujaribu