Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool yampandia dau Isak

Muktasari:

  • Kiasi hicho cha pesa kinaonekana kuwa kitavunja rekodi ya usajili ya England pamoja na mjumuisho wa nyongeza yake.

Liverpool inajiandaa kutoa ofa ya Pauni 130 milioni kwenda Newcastle United kwa ajili ya kumsajili straika wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Sweden Alexander Isak, 25, katika dirisha hili.

Kiasi hicho cha pesa kinaonekana kuwa kitavunja rekodi ya usajili ya England pamoja na mjumuisho wa nyongeza yake.

Liverpool inataka kumsajili Isak ili kuziba pengo la Darwin Nunez ambaye ametimkia Al-Hilal ya Saudi Arabia katika dirisha hili.

Mabosi wa Newcastle walijaribu kwenda nyumbani kwa Isak kwa ajili ya kuzungumza naye ili kumshawishi arejee katika kikosi, lakini bado alikataa na kusisitiza kwamba anahitaji kuondoka na kutua Liverpool.

Liverpool inataka kutoa ofa tajwa hapo juu kabla ya dirisha kufungwa na endapo itakataliwa haitaongeza tena pesa nyingine.

Newcastle inadaiwa kuhitaji kiasi kisichopungua Pauni 150 milioni ili kumuuza Isak pesa ambazo ni ngumu kutolewa na Liverpool kwa sasa.

Mkataba wa sasa wa Isak unatarajiwa kumalizika mwaka 2028 na msimu uliopita alicheza mechi 42 za michuano yote, akafunga mabao 27 na kutoa asisti sita.


Rasmus Hojlund

Manchester United imekubali kumtoa mshambuliaji wake wa kimataifa wa Denmark, Rasmus Hojlund, 22, kwa mkopo wa msimu mzima kwenda Napoli, huku kukiwa na kipengele cha kumnunua kwa takribani Pauni 38 milioni mwisho wa msimu kama atacheza idadi fulani ya mechi. Hojlund alisajiliwa na United kutoka Atalanta mwaka 2023 kwa zaidi ya Pauni 72 milioni na Napoli inamwona kama mrithi sahihi wa Victor Osimhen aliyetimkia Galatasaray.


Maximilian Beier

Brentford imegonga mwamba katika mpango wa kutaka kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Ujerumani, Maximilian Beier, 22, baada ya ofa yao ya Pauni 45 milioni kukataliwa.

Beier alifunga mabao 16 akiwa na Hoffenheim msimu wa 2023/24 kabla ya kujiunga na Dortmund katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi.


Tyrique George

AS Roma imewasilisha ombi kwa ajili ya kumnasa kinda wa Chelsea, Tyrique George, 19, katika dirisha hili.

George ni sehemu ya timu ya vijana ya England wenye umri chini ya miaka 20.

Hata hivyo, inakumbana na upinzani mkubwa kutoka kwa Bayern Munich, Fulham na Crystal Palace ambazo pia zinahitaji huduma yake.

Mabosi wa Chelsea wanahitaji kiasi kisichopungua Pauni 20 milioni ili kumuuza lakini ripoti zinadai pia itakuwa tayari kumtoa kwa mkopo.


Manuel Akanji

AC Milan inataka kumsajili beki kisiki wa Manchester City na timu ya taifa ya Uswisi, Manuel Akanji, 30, katika dirisha hili la majira ya kiangazi.

Staa huyu ni miongoni mwa wachezaji ambao Crystal Palace pia wanavutiwa naye na inahitaji kumsajili katika dirisha hili la majira ya kiangazi. Milan inamwona staa huyu kama mbadala wa beki wake, Simon Kjaer.

Mbali ya Milan, timu kadhaa za England pia zinahitaji huduma yake lakini hadi sasa bado Akanji hajafanya uamuzi wa wapi atatua.


Axel Disasi

Beki kisiki wa Chelsea, Axel Disasi mwenye umri wa miaka 27, yupo katika rada klabu yake ya zamani AS Monaco, inayotaka kumsajili kwa mkopo wa msimu mmoja. Bournemouth na Aston Villa pia ni kati ya timu zinazomfuatilia beki huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa. Disasi ni miongoni mwa wachezaji ambao hawapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha Chelsea hali inayosababisha aombe kuondoka.


Kostas Tsimikas

Liverpool na Roma zipo katika mchakato wa mwisho kukamilisha dili la beki wa kushoto wa Liverpool, Kostas Tsimikas katika dirisha hili. Tsimikas mwenye umri wa miaka 29, amecheza kwa misimu minne akiwa na Liverpool ambapo kiujumla amecheza mechi 70. Roma ipo tayari kutoa Euro 25 milioni kwa ajili ya kumnunua staa huyu wa kimataifa wa Ugiriki. Mkataba wake unaisha 2027.


Oleksandr Zinchenko

Marseille inamnyemelea beki wa Arsenal na timu ya taifa ya Ukraine, Oleksandr Zinchenko, 28, ikihitaji kumsajili katika dirisha hili la majira ya kiangazi. Hata hivyo, dili hilo linaonekana kuchelewa kwa sababu Zinchenko anataka mshahara wa Pauni 120,000 kwa wiki kiasi ambacho Marseille wanaona ni kikubwa. Staa huyo ameomba kuondoka Arsenal.