Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Isak, Guehi watengewa kitita Liverpool

ISAK Pict

Muktasari:

  • Kiasi hicho cha pesa kimetengwa kwa ajili ya usajili wa Alexander Isak  na Marc Guehi ambao kuna zaidi ya asilimia 70 za kuwapata.

Liverpool, England. Liverpool iko tayari kufanya ununuzi mkubwa wa zaidi ya Pauni 150 milioni wa wachezaji kabla ya dirisha hili la uhamisho la majira ya kiangazi kufungwa.

Kiasi hicho cha pesa kimetengwa kwa ajili ya usajili wa Alexander Isak  na Marc Guehi ambao kuna zaidi ya asilimia 70 za kuwapata.

Isak ameweka wazi kuwa  yuko tayari kuondoka na kutua Liverpool na inaonekana ni kama Newcastle imeanza kujiandaa na maisha bila ya yeye kwani inapambana kumpata mshambuliaji wa  Wolves, Jorgen Strand Larsen ambaye imeshatuma ofa mara mbili kwa ajili yake lakini zimekataliwa.

Mchezaji mwingine ni  nahodha wa Crystal Palace, Guehi, ambaye taarifa zinaeleza kuna uwezekano akauzwa kabla ya dirisha la usajili kufungwa  Jumatatu.

Palace inadaiwa kuiambia Liverpool, inataka kumaliza mechi ya kucheza kufuzu Kombe la Europa Conference kesho, Jumamosi  dhidi ya Fredrikstad kabla ya kumuuza.

Kaimu mwenyekiti wa Palace, Steve Parish, anadaiwa kuhitaji walau Pauni 40 milioni kwa ajili ya kumuuza Guehi ambaye amebakisha mwaka mmoja tu katika  mkataba wake wa sasa, lakini Liverpool wana uhakika kwamba wanaweza kumpata kwa bei ya chini.

Awali Man City ilikuwa ikihitaji huduma ya Guehi lakini sasa Liverpool pekee ndio inaonekana kubakia katika harakati hizo.

Katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi, Palace ilikataa ofa inayokaribia Pauni 70 milioni lakini sasa italazimika kumuuza tu kwa sababu haitaki kuona akiondoka bure mwisho wa msimu.

Newcastle tayari imekataa ofa moja ya Pauni 110 milioni na kusisitiza kuwa inahitaji Pauni 150 milioni kwa ajili ya Isak ingawa inaaminika kuwa Liverpool kiasi chao cha mwisho inachohitaji kulipa ni Pauni 130 milioni.

Isak, ambaye amekuwa akifanya mazoezi peke yake tangu kwa muda sasa, hajacheza katika mechi za mwanzo mbili za ligi za Newcastle lakini anatarajiwa kuwepo katika mechi za  kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Slovenia na Kosovo mwezi ujao.