Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu Isak kuhama nyumba ya kifahari yafichuka

Muktasari:

  • Howe angetamani mchezaji huyo abadili mawazo na kusalia klabuni, lakini anaelewa nafasi ya jambo hilo kutokea ni ndogo.

London, England. Mshambuliaji wa Newcastle United, Alexander Isak, amehamia makazi mapya, huku taarifa zikithibitisha kuwa uamuzi huo hauna uhusiano wa moja kwa moja na nia yake ya kutaka kujiunga na Liverpool.

Isak, raia wa Sweden, amekuwa akiishi kwenye nyumba ya kifahari yenye vyumba vinne vya kulala katika eneo la Darras Hall, Northumberland, tangu ajiunge na Newcastle mwaka 2022 akitokea Real Sociedad kwa ada ya pauni milioni 63. Nyumba hiyo aliyokuwa akiikodi kwa zaidi ya pauni 7,000 (Sh24 milioni) kwa mwezi, ilihusisha jiko la kisasa, sebule ya wazi na chumba cha burudani.

Hata hivyo, majirani wamesema Isak alikuwa amepanga kuondoka baada ya kuvamiwa nyumbani kwake mara mbili, tukio lililomwacha na hofu kubwa ya usalama. Mwezi Mei mwaka huu, familia ya watu wanne ilihukumiwa kifungo baada ya kuhusika na wizi huo.

Kwa mujibu wa taarifa za mahakamani, wavamizi hao waliiba gari la michezo la Isak, vito vyenye thamani ya pauni 68,000 na fedha taslimu kati ya pauni 8,000 hadi 10,000. Isak alieleza kuwa uvamizi wa kwanza ulikuwa Aprili 4, 2024 aliporejea nyumbani na kukuta gari lake limeibwa.

“Shambulio hili limeniacha na hali ya wasiwasi mkubwa na hofu ya kutokea tena,” alisema Isak katika taarifa yake.

Kutokana na mfululizo wa wizi kwa wachezaji, Newcastle ililazimika kuimarisha ulinzi kwa kufunga mitambo ya tahadhari inayofuatiliwa na doria za usalama.

Kwa sasa, mustakabali wa Isak umeendelea kutawala vichwa vya habari vya dirisha la usajili. Ameshawaambia Newcastle na kocha Eddie Howe kwamba anataka kujiunga na Liverpool. Hata hivyo, uhamisho huo hautakamilika hadi Newcastle watakapopata mshambuliaji mbadala na Liverpool kurejea na ofa inayokubalika baada ya ile ya pauni milioni 110 kukataliwa mapema mwezi huu.

Howe angetamani mchezaji huyo abadili mawazo na kusalia klabuni, lakini anaelewa nafasi ya jambo hilo kutokea ni ndogo.