Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Morocco aeleza walivyojiandaa kuizima Comoro

Muktasari:

  • Shambulizi la kwanza lilikuja ndani ya dakika tano za mwanzo, Selemani alipochukua mpira uliokuwa unazagaa zagaa katika eneo la Morocco lakini alishindwa kuuweka kimiani.

Rabat, Morocco. Kocha wa timu ya Morocco, Walid Regragui amesema walitumia muda wa mwaka mmoja na nusu kujiandaa na mchezo dhidi ya Comoro na matokeo yameonekana.

Morocco jana ilianza kampeni yake ya Kombe la Mataifa ya Afrika la CAF (TotalEnergies) 2025 kwa ushindi wa 2–0 dhidi ya Comoros, katika mechi iliyochezwa mbele mashabiki wengi kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdellah, Rabat, Jumapili usiku.

Mabao ya kipindi cha pili kutoka kwa Brahim Díaz na Ayoub El Kaabi yalitosha kuamua matokeo ya mchezo ambao ulikuwa mgumu zaidi kuliko inavyoonyesha matokeo, huku wenyeji wakilazimika kuwa na subira dhidi ya Comoros waliocheza kwa nidhamu na uthabiti ya ulinzi.

Tangu mwanzo, Morocco ilitawala umiliki wa mpira, ikipiga pasi kwa kujiamini na kuwasukuma Comoros wajilinde ndani ya nusu yao. Hata hivyo, nafasi za wazi zilikuwa chache mwanzoni kutokana na ulinzi imara wa wageni.

Onyo la kwanza lilikuja ndani ya dakika tano za mwanzo, Selemani alipochukua mpira uliokuwa unazagaa zagaa katika eneo la Morocco lakini alishindwa kuuweka kiminiani.

Atlas Lions walidhani wamepata bao la mapema baada ya Brahim Díaz kuingia kwenye eneo la hatari na kuchezewa faulo iliyozalisha penalti. Hata hivyo, kipa Yannick Pandor alisoma vizuri mwelekeo wa mpira na kuokoa mkwaju wa Soufiane Rahimi ambaye awali alikuwa amepiga penalti tisa bila kukosa hata moja.

Kukosa huko kuliwavuruga kidogo wenyeji, ambao waliendelea kushambulia kupitia mipira ya adhabu na krosi. Ismaël Saibari alipiga kichwa kilichopita karibu na lango, huku Azzedine Ounahi akimjaribu kipa wa Comoros kwa shuti la mbali, lakini alionyesha uwezo wa juu.

Kipindi cha kwanza pia kiligubikwa na jeraha la mapema kwa nahodha Romain Saïss, aliyelazimika kutoka uwanjani baada ya kugongana vibaya na kuumia nyama za paja.

Bao la kufungua pazia lilipatikana dakika kumi baada ya kuanza kwa kipindi cha pili. Shambulizi zuri kutoka upande wa kushoto lilimaliziwa na Noussair Mazraoui aliyepiga krosi ya chini ndani ya boksi, ambapo Brahim Díaz alifika kwa wakati sahihi na kumalizia kwa utulivu mpira uliompita Pandor, na kuamsha shangwe uwanjani.

Baada ya hapo Morocco ilianza kucheza kwa uhuru zaidi. Comoros waliendelea kupambana, lakini mianya ilianza kuonekana.

Dakika ya 73 Ayoub El Kaabi aliyeingia kuongeza makali alifanya kazi ya kipekee kwa kupiga mpira wa akrobatiki (overhead kick) akimalizia pasi kutoka kwa Salah-Eddine, na kumuacha kipa bila jibu na kufunga bao ambalo linatabiriwa kuwa bora la mashindano hadi sasa.

Walid Regragui kocha wa Morocco baada ya mechi hiyo alisema“Tumejiandaa kwa mchezo huu kwa mwaka mmoja na nusu. Tuliweka shinikizo kubwa juu yetu. Tulianza vibaya kidogo, penalti iliyokoswa na jeraha la Romain Saïss. Wakati wa mapumziko sikuridhika sana na timu, tukazungumza na kufanya marekebisho fulani ambayo wachezaji walitekeleza haraka sana na matokeo yameonekana.”

wakati akisema hivyo, kocha wa Morocco Stefano Cusin yeye alisema kuwa:

“Tulikuwa imara katika ulinzi. Lakini katika michezo ya aina hii, fursa inapokuja lazima uitumie. Timu ilionyesha sura nzuri, na wananchi wa Comoros wanaweza kujivunia nchi yao. Hatuwezi kusema tulicheza vibaya kwa sababu tu tuliruhusu mabao mawili. Kama Rafiki angefunga na kufanya 1–1, hali ingeweza kuwa tofauti. Morocco ni timu kubwa; tunapaswa kukubali kushindwa dhidi ya timu ya kiwango hicho.”